PreGE2025 Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) yasisitiza haitaongeza siku za uboreshaji awamu ya pili

PreGE2025 Tume Huru ya Uchaguzi(INEC) yasisitiza haitaongeza siku za uboreshaji awamu ya pili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
262
Reaction score
297
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mzunguko wa pili ulioanza Mei 16 hadi22, 2025 ukikamilika Tume haitaongeza siku za ziada hivyo wananchi wenye sifa wajitokeze katika siku mbili zilizobaki kujiandikisha au kuboresha taarifa zao na kuwaondoa wale wasio na sifa kuwepo kwenye Daftari hilo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani Mhe. JACOBS MWAMBEGELE wakati wa ziara ya kukagua mwenendo wa zoezi hilo la Uboreshaji na uwekaji wazi Daftari la awali katika Halmashauri za Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga yenye majimbo ya Uchaguzi ya Lushoto na Mlalo.

 
Back
Top Bottom