Tume huru ya uchaguzi iweje?

Tume huru ya uchaguzi iweje?

luchili

Senior Member
Joined
Nov 30, 2018
Posts
131
Reaction score
54
Tumekuwa tukiwasikia viongozi wa Vyama vya Upinzani wakidai Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 uwe wa haki na huru. Sasa najaribu kutafakari, hawa vyama pinzani wataona uchaguzi wa 2020 kuwa upo huru na haki endapo watausimamia wenyewe?

Maana inafahamika sheria na taratibu za uchaguzi zilivyo na katiba yetu inajieleza pia. Jamani wakati mwingine tufikie hatua tukubaliane na utaratibu tuliojiwekea wenyewe na hata Rais Magufuli ameuthibitishia umma kuwa uchaguzi 2020 utakuwa wa huru na haki, tuelewe tu na kuaminiana.

Wapinzani wasije wakaona uchaguzi 2020 amechaguliwa Magufuli tena, wakaanza na mambo yao ya kusema uchaguzi haukuwa wa uhuru na haki,watambue tu Magufuli anapendwa na kila rika.
 
Mchakato wa uchaguzi ndio unaorasimisha au unaoharamisha kuwa uchaguzi ni huru na wa haki mengine bla blah tu. Mchakato wa uchaguzi Tanzania unaonesha ni uchaguzi wa haki.
 
Hoja hii ngoja ijibiwe na iliyo bora zaidi,kwa hiyo mtoa hoja unaona ni haki kabisa kwa political cadres walioteuliwa na chama dola kusimamia uchaguzi kuwa watausimamia uchaguzi huu kwa haki?,unaona na haki kwa our no 1 kuteua makamishina wa NEC kusimamia uchaguzi kwa haki wakati aliyewateua na chairman wa chama cha kisiasa?

Mbona hujiulizi kuwa tume hii ipo kwenye ngazi ya taifa tu,lakini haipo kwenye ngazi ya mikoa hadi mitaani(huku uchaguzi huu unasimamiwa na ma comrades wa chama dola!!)ungekuwa unapenda kujisomea na kuongea Facts ningekuomba angalia muundo wa tume ya uchaguzi ya Kenya,Namibia,Botswana,na RSA halafu linganisha na mfumo wetu,elewa tume ya uchaguzi ya RSA haitakuja kuwa na mwenyekiti ambaye ni jaji(maana kutakuwa na conflicts of interest kama matokeo yatakuwa challenged mahakamani),tuendelee kusubiri generation yenye balls,sisi tuendelee kulalama kwenye keyboards za JF.
 
Tumekuwa tukiwasikia viongozi wa Vyama vya Upinzani wakidai Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 uwe wa haki na huru. Sasa najaribu kutafakari, hawa vyama pinzani wataona uchaguzi wa 2020 kuwa upo huru na haki endapo watausimamia wenyewe?

Maana inafahamika sheria na taratibu za uchaguzi zilivyo na katiba yetu inajieleza pia. Jamani wakati mwingine tufikie hatua tukubaliane na utaratibu tuliojiwekea wenyewe na hata Rais Magufuli ameuthibitishia umma kuwa uchaguzi 2020 utakuwa wa huru na haki, tuelewe tu na kuaminiana.

Wapinzani wasije wakaona uchaguzi 2020 amechaguliwa Magufuli tena, wakaanza na mambo yao ya kusema uchaguzi haukuwa wa uhuru na haki,watambue tu Magufuli anapendwa na kila rika.
Unauliza maswali ya kijinga. Unaelewa maana ya neutrality and conflict of interest?
 
Kwanza jina lake tu liwe ni TUME HURU YA UCHAGUZI
Viongozi wake wapatikane kwa njia ya ushindani wa wazi, kazi zao kuanzia Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe/makamishna wa tume zitangazwe na waombe kupitia kwa katibu wa Bunge, wafanyiwe usahili na Bunge na waapishwe na Jaji Mkuu, na wasiripoti kwa mtu yeyote,
Tume iwe na watumishi wake wengine wa kudumu ambao hawapaswi kuwa wafuasi wa chama chochote cha siasa.
Tume iwe inapewa fedha zake mojakwa moja na hazina kupitia kwa CAG
 
Na makamishna wa tume huru ya uchaguzi wawe na security of tenure siyo kuteuliwa na kufukuzwa pasipo na sababu za kisheria na kikatiba ktk utumishi wao. Tume huru ndiyo itasimamia chaguzi zote ktk ngazi kuanzia mitaani mpk taifa siyo wizara ya tamisemi ambayo viongozi wake ni makada wa chama cha siasa ambacho ni mshindani! Sawa na mechi ya simba na yanga umpe mwenyekiti wa simba jukumu la kuteua refa na washika vibendera na makamisaa. Mwisho tume iwajibishwe mahakamani pindi inakosea ktk utendaji kazi na maamuzi - no immunity.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lako tu linaonesha hujiamini kwamba Ccm haiwezi kushinda hata ubalozi wa nyumba 10 bila kutumia TISS, Police na vyombo vingine! Chama kinachojinasibu kupendwa kinaogopa Marefa huru? Ni sawa na ati leo liverpool ianze kuogopa marefa toka mataifa mengine wakati inaongoza ligi?
Tumekuwa tukiwasikia viongozi wa Vyama vya Upinzani wakidai Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 uwe wa haki na huru. Sasa najaribu kutafakari, hawa vyama pinzani wataona uchaguzi wa 2020 kuwa upo huru na haki endapo watausimamia wenyewe?

Maana inafahamika sheria na taratibu za uchaguzi zilivyo na katiba yetu inajieleza pia. Jamani wakati mwingine tufikie hatua tukubaliane na utaratibu tuliojiwekea wenyewe na hata Rais Magufuli ameuthibitishia umma kuwa uchaguzi 2020 utakuwa wa huru na haki, tuelewe tu na kuaminiana.

Wapinzani wasije wakaona uchaguzi 2020 amechaguliwa Magufuli tena, wakaanza na mambo yao ya kusema uchaguzi haukuwa wa uhuru na haki,watambue tu Magufuli anapendwa na kila rika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamooni wakuu.
Kila siku nasikia watu wanalilia tume huru. Nimewaza kwa ka akili kangu juu ya tume huru kwa maswali yafutayo.
1. Je, hii tume huru mnaamaanisha nini?
2. Je, kama mahakama mnayosema ipo huru na wengine wanasema haipo huru, je hiyo tume itakuwa huru kweli?
3. Je, kuna Watu ambao hawana upande (neutral) watakaofaa kwenye hiyo tume?
4. Je, fedha ya hiyo tume itakuwa huru?
5. Je, kama tume ya uchaguzi ya marekani ambayo inaonekana ni huru na bado kuna malalamiko ya uchaguzi kuingiliwa na Urusi, je itawezekana Nchini mwetu?
6. Je, siasa yetu inamtazamo upi juu wa hiyo tume huru?

Mimi sielewi chochote kabisa, nisaidieni kuelewa.
 
Attachments

  • 78415996_2778911385485033_1590029126708756480_o.jpg
    78415996_2778911385485033_1590029126708756480_o.jpg
    192.4 KB · Views: 2
Tume huru ni ile itakayoruhuru watu kujumlisha kura za urais na kuhakiki kama matokeo yaliyotangazwa ni sawa.
 
Back
Top Bottom