Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania iige mfano wa Kenya

Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania iige mfano wa Kenya

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Nchi ya Tanzania inatakiwa iige utaratibu wa Tume Huru ya Kenya. Kupata Mwenyekiti na Makamishna wa Uchaguzi wanatakiwa wapatikane kwa njia ya haki. Mfano wiki hii kule Kenya wametangaza nafasi ya Mwenyekiti na Makamishna wa Tume Huru ya Kenya na sharti ni kuwa anayetaka nafasi hizo ni lazima atume maombi.

Kufikia jana walioomba nafasi hizo wamefikia zaidi ya elfu tatu na ushehe. Kwa Tanzania tunatakiwa nafasi hizi zitangazwe na watu waombe na wafanyiwe usaili na wale watakoonekana wanafaa basi wachaguliwe na hapo hapatakuwa na malalamiko toka kwa wapinzani.

Kwa wale wanaosimamia usaili basi kila Chama kipendekeze mtu wao wa kuingia katika jopo la usaili ili kuwe na haki.

Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya imewaajiri watumishi wake nchi nzima na sisi tuige mfano wao ambao Tume Huru ya Uchaguzi iajiri watumishi wake kwa ajili ya chaguzi zote na hapa wapinzani hawatapata nafasi ya kulalalmika. Hebu tujifunze kutoka kwa wenzetu wa Kenya.
 
Back
Top Bottom