Tume imeelemewa na shuhuda za kweli. Sasa hawataki tena ziende hewani moja kwa moja

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kwanza iliundwa kimkakati sana

Hakukuwa mjumbe hata mmoja nje ya cycle yao.. Wajumbe wote ni makada watiifu wenye maisha mazuri kupitiliza

Pili jina lililopewa lilimaanisha kuinasua serikali na tuhuma za mauaji na kuwasakizia wananchi kuwa ndio walifanya vurugu

Uongo hupanda lift bali ukweli hukwea ngazi. Wakati ni hakimu wa haki.. Kinachotokea kwenye shuhuda kinatisha na kuumiza zaidi

Japo watu wengi walisusia kufika mbele ya tume ya mchongo lakini hao kiduchu waliofika wamivua nguo serikali na mamlaka zake!

Tume imelemewa na shuhuda za kweli sasa hawataki tena ziende hewani moja kwa moja.. Waandishi wamezuiwa kuripoti direct na sasa watasubiri watakachopewa na tume
Tunarudia tena kosa like lile.. Kukipaka kinyesi manukato ili ksinuke
 
Wamepewa maelekezo kutoka juu
 
Swali ni moja tu, ikiwa sisi wazazi tulishindwa kuwazuia watoto wetu wasiandamane adhabu yao ilikuwa ni kifo??

Ikiwa vijana wetu walipewa fedha ili waandamane adhabu yao ilikuwa ni kuuawa kwa kufumuliwa ubongo??

Hawana namna ya kutoka kwenye mkasa huu. Ni kweli wao ndio wauaji wa raia. Sasa Tume ya nini??

Mama mwenyewe keshakiri kwa kusema " mlitaka tuwatizame waliotaka kupindua Serikali hadi wafanikiwe?"
 
Yameanza kuwatokea puani
 
Yule bibi aliepigwa risasi, sikumfatilia VIZURI, kumbe yule member anae SEMA bibi muongo ni CHAWA, bibi KASEMA jamaa walienda hospital wakawa wanauliza wagonjwa kama umepiga kura au huja piga, wanakagua vidole,kama Kuna wino, kitima ALISEMA JAMAA walienda KUUA hospitalini majeruhi Sasa HAPO uongo WA bibi UKO WAPI. Uongo WA kitima UKO WAPI?
 
Na hii ndio sababu ya kusitisha live coverage
 
Mama nwenyewe keshakiri kwa kusema " mlitaka tuwatizame waliotaka kupindua Serikali hadi wafanikiwe?"
 
Laana kubwa sana
 
Tume ya mchongo.
 
Watatumia sabuni gani kusafisha uchafu huo iwapo utakuwa wazi kwa waTanzania wote?

Wakiruhusu uwazi tayari watakuwa wamekinzana na lengo la kazi yao waliyopewa. kuitimiza.

Ninawahofia tu hao wanaojitokeza kwenye tume hiyo kutoa ushuhuda; wanaweza kuwa wanajiweka hatarini bila kujuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…