DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU KUSITISHA UCHAGUZI KATIKA KATA YA KIRUA VUNJO MAGHARIBI
Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.
Kwa kuzingatia masharti ya Kifungu cha 71(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 na kwa barua yenye Kumb. Na CMV/U.30/10/VOL.II/45 ya tarehe 21 Oktoba, 2025 kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi nimepokea taarifa ya kifo cha Ndugu John Boniface Kessy aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Udiwani Kata ya Kirua Vunjo Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi.
Kutokana na kutokea kwa kifo hicho, Uchaguzi wa Udiwani katika Kata ya Kirua Vunjo Magharibi Jimbo la Vunjo UMESITISHWA kuanzia 21 Oktoba, 2025. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 71(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itatoa notisi itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali na itapanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea ambapo taratibu za uchaguzi wa Udiwani katika Kata husika zitaanza upya.
Hivyo, uteuzi wa wagombea katika kata ya Kirua Vunjo Magharibi na taratibu za uchaguzi zitaanza upya.
Pia Soma: TANZIA - Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Kirua Vunjo Magharibi, John Kessy, afariki Dunia. Uchaguzi waahirishwa