A
Anonymous
Guest
“Tume ya Jaji Lila ni ukuta unaojengwa kwenye msingi ulioandaliwa na Tume ya awali ya kutambua vyanzo vya vurugu za Oktoba 29, 2025, iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman Chande. Kama taarifa kwa vyombo vya habari inavyoeleza, Tume ya Jaji Lila ni utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande,”
Anasema Jesse Kwayo mwahabari wa muda mrefu katika andiko lake lililochapidhwa mara baada ya kutangazwa kwa kuundwa kwa Tume hiyo. Nukuu hiyo inatupa msingi wa uchambuzi.
Tume ya Jaji Lila ni Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 nchini Tanzania, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji wa Mahakama ya Rufani mstaafu, Shabani Ally Lila. Tume hiyo inaundwa na makamishna watatu ambao ni majaji wastaafu wa Mahakama Kuu: Jaji mstaafu Gad John Mjemmas, Jaji mstaafu Awadh Mohamed Bawazir na Jaji mstaafu Aishieli Nelson Sumari.
Tume hiyo iliundwa na Rais Samia Suluhu Hassan mnamo Mei 18, 2026, kufuatia mapendekezo ya Tume ya Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande kuhusu ghasia za Oktoba 29, 2025.
Hata hivyo, ilikumbana na ukosoaji kutoka kwa wadau, ikiwamo kesi iliyofunguliwa mahakamani kupinga uhalali wa tume hiyo. Mnamo Julai 17, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia Jaji Wilbert Chuma, ilitupilia mbali shauri hilo, ikieleza kuwa lililetwa kabla ya wakati na kukosa mashiko.
Kufuatia uamuzi huo, Rais Samia alizindua rasmi Tume hiyo ili ianze kufanya kazi kwa kipindi cha siku 150.
Kwa sasa, zimepita zaidi ya siku 60 tangu Tume hiyo ianze kufanya kazi. Ilipewa jukumu la kuchunguza na kuwabaini watu binafsi au makundi yaliyopanga, kuratibu, kufadhili au kutekeleza ghasia hizo, pamoja na kuchunguza kiwango cha nguvu kilichotumika kudhibiti ghasia hizo.
Tume imekuwa ikiendelea kuzunguka katika wilaya mbalimbali, kama vile Ubungo na Temeke, na sasa ipo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Maendeleo ya tume (mtazamo)
Kutokana na ufuatiliaji tangu Tume hiyo ianze kutekeleza majukumu yake, kuna mambo kadhaa yanayoweza kuibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa Tume hiyo kuvuka kivuli cha Tume ya Jaji Chande, ambayo iliacha gumzo na ukosoaji mkubwa uliohusu matumaini, matarajio na imani kuhusu uwajibikaji wa kweli katika tume zinazoundwa.
Kivuli hiki kimetanda katika mitazamo ya wadau wa haki, baadhi ya vyama vya siasa na wananchi, pamoja na mijadala kwenye mitandao ya kijamii.
Mambo niliyobaini hadi sasa
Mwitikio mdogo wa wadau: Katika nyakati tofauti nilizofika eneo la Ubungo, ambako Tume hiyo ilikuwa ikipokea taarifa na ushahidi mbalimbali, kumekuwa na mwitikio mdogo huku hamasa ikiwa chini, licha ya Mkuu wa Wilaya, Msando, kutoa rai kwa wadau na wananchi wenye taarifa kujitokeza. Nimedokezwa kuwa hali hiyo pia imejitokeza katika baadhi ya maeneo mengine.
Kupotea kwenye mijadala ya umma: Wakati Tume ya Jaji Chande ilipoundwa, licha ya kuwepo kwa ukosoaji, iliweza kuteka hisia za watu na kuwa sehemu ya mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo nyakati ilipokuwa ikikusanya ushahidi. Hata hivyo, kwa sasa ni nadra kuikuta Tume ya Jaji Lila ikitawala au kuwa sehemu kuu ya mijadala hiyo. Huenda jambo hilo lina tafsiri mbili, lakini linaleta wasiwasi kuhusu mtazamo wa jamii.
Hapo ndipo hoja ya kivuli cha ripoti ya Jaji Chande inapojitokeza. Wapo wadau wanaoamini kuwa ripoti ya Jaji Chande, pamoja na suala la uwajibikaji baada ya ripoti kutolewa, imezika matumaini ya umma kuhusu uwajibikaji unaopitia katika tume za ndani zinazoundwa na mamlaka za juu.
Kukosa kipaumbele kwenye vyombo vya habari: Licha ya Tume hiyo kuelezwa kuwa ni tume huru isiyoingiliwa, ilitarajiwa kuwa utendaji wake ungepewa uzito katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, ikizingatiwa kuwa inalenga kuweka wazi wahusika wa matukio yaliyoripotiwa kutokea.
Kutokana na ufuatiliaji wangu, vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi bado havitoi uzito wa kihabari unaostahili wakati Tume hiyo ikiendelea na hatua za uchunguzi. Jambo hilo linaweza kuibua hoja kwamba uzito wa maslahi ya umma, ambao vyombo vingi vya habari vinapaswa kuupa kipaumbele, haupo au umefifia kwa Tume hiyo. Hilo ni suala linaloweza kutupa tafakari na kuibua mjadala.
Ukosoaji wa wadau: Baadhi ya wadau, ikiwamo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekuwa wakikosoa muundo wa Tume hiyo kwa nyakati tofauti. Kupitia viongozi wake, chama hicho kimekuwa kikiikosoa Tume hiyo na kueleza kuwa umma hauna imani nayo.
Akiwasilisha maazimio ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Septemba 19, 2026, Dkt. Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, alisema: “Kamati Kuu inasema kile kilicholengwa na Tume ya Jaji Lila ni kutaka kusafisha watawala na Serikali iliyopo madarakani ya Rais Samia na kuwabambikia watu wengine na mauaji au vurugu zile za Oktoba 29.”
Matarajio yanayohusishwa na mwenendo wa kisiasa: Baadhi ya wanaharakati na wadau wamekuwa wakihusisha kuundwa kwa Tume hiyo na uwezekano wa kutumiwa kama nyenzo ya kuwajibisha wakosoaji wa Serikali badala ya kusimamia ukweli na uhalisia wa mambo yalivyotokea.
Hoja za wadau zinaenda mbali zaidi, zikitabiri baadhi ya majina ya watu wanaodaiwa kulengwa ili wabebeshwe mzigo wa matukio ya Oktoba 29, 2025. Jambo hilo linaweza kuiweka Tume katika mazingira yenye presha, huku likiacha maswali na kupunguza imani ya baadhi ya watu wanaoiona kama tume ya kisiasa.
Muda wa Tume kufanya kazi na kukabidhi ripoti: Muda wa miezi mitano uliopewa Tume hiyo kufanya kazi ni sehemu ya wasiwasi unaoweza kupelekea jamii kupunguza imani na kuungana na kauli za baadhi ya wanaharakati na wadau wanaodai kuwa Tume hiyo ni ya kisiasa.
Hoja ya muda mrefu wa uchunguzi ilijitokeza pia wakati wa Tume ya Jaji Chande, ambapo baadhi ya wananchi waliamini kuwa huenda ulikuwa sehemu ya kupoteza muda na kuifanya jamii isahau yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Athari za masuala hayo
Masuala hayo, kwa namna moja au nyingine, yanaweza kuathiri ripoti ya Tume pamoja na namna wananchi watakavyoikubali baada ya kutolewa.
Tume hii inabaki katika mtego mzito wa kiimani ambao unaweza kuathiri mwelekeo mpya wa kijamii na kitaifa. Dhamira ya kweli inahitajika ili kufifisha kivuli cha mashaka na kurejesha imani na matumaini. Je, hilo litawezekana?
Mwisho: Tume hiyo kwa nyakati tofauti imeendelea kutoa wito kupia Jaji Lila ikiwataka wananchi wenye taarifa zinazohusiana na Hadidu Rejea za Tume kujitokeza na kuwasilisha taarifa hizo ili kusaidia uchunguzi.