Tume ya katiba lindeni amani ya nchi

Tume ya katiba lindeni amani ya nchi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Tanzania tumebahatika kuwa na amani kwa mda mrefu ingawa kwa sasa viashiria vibaya vinaanza kuibuka. mambo ambayo yamekuwa yakivunja amani katika nchi nyingi ni pamoja na siasa za nchi, rasilimali za nchi na imani za watu. Wakati huu wa kuunda katiba mpya ndio wakati muafaka wa kulinda amani ya nchi kwa kutumia katiba ya nchi. Kuhusu siasa tunaanza kuona jinsi siasa za Tanzania zinavyoanza kuchafuka. Siri kubwa ya rasilimali zilizoko kwenye siasa zinazopelekea watu kuvurugana mpaka wengine kukimbilia msituni au kuanza kufanya vitendo vya kigaidi ni madaraka ya raisi hasa katika teuzi mbalimbali. nafasi hizi za teuzi ndizo zinasababisha watu kuunda mitandao ya uraisi, nafasi hizi ndizo zinazopelekea watu kukimbilia msituni wakiangalia tukifanikiwa katika uteuzi nitapewa cheo. Kwa nini tuzidi kulea mfumo huu unaoangaisha watu kuwaondolea amani huku ukidumaza maendeleo ya watu kwa kuwateua watu kulipa fadhila na kukuta watu wakishikilia nyadhifa wasizozimudu na wanapokosea hubadilishwa nyadhifa kama ndio njia ya kuwawajibisha kwa sababu ni wana mtandao. Tunaomba tume ya katiba nafasi nyingi za utendaji ziondolewe katika uteuzi wa raisi ziwekwe katika mfumo wa watanzania wenye sifa kugombania Raisi abaki na baraza la mawaziri tu na hao wawe na sifa za ujuzi na uzoefu. hapa tutaondoa kwa kiasi kikubwa waleta chokochoko katika siasa zetu. Lakini pia rasilimali za taifa zimekuwa zikiporwa na wenye dhamana huku taifa likipoteza rasilimali. tunaomba katiba itoe asilimia ya mapato ghafi ambayo kwa mgeni yeyote anayetaka kuja kuwekeza Tanzania haipaswi kushuka asilimia Fulani ya mapato ghafi na kama inaonekana wawekezaji wanashindwa basi ziachwe watanzania wakiwa na uwezo watavuna wenyewe. tatu katiba itamke wazi kuwa Tanzania haina dini hivyo serikali itatoa nafasi kwa watu kufuata imani zao lakini serikali yenyewe haitajihusisha na shughuli za imani yoyote.
 
Back
Top Bottom