Naumiza kichwa mpaka sasa sijui mh rais ametumia kigezo gani kupata hii tume?
Zanzibar ni nchi hivyo ni lazima iwe na wajumbe sawa na nchi ya Tanganyika!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naumiza kichwa mpaka sasa sijui mh rais ametumia kigezo gani kupata hii tume?
Zanzibar ni nchi hivyo ni lazima iwe na wajumbe sawa na nchi ya Tanganyika!!
Sasa tunalo hili la Ratio ya Bara na Visiwani na uislam; sitashangaa likiibuka na suala la jinsia tutasema wanawake ni wachache mawazo yao yatamezwa na wanaume, kama haitoshi tutaanza kuyachambua na makabila, ili tujue ni kabila gani wako wengi kuliko jingine; ni mwanzo wa kubaguana hebu tuipe baraka TUME hii ifanye kazi yake kwa uzuri na hata wakija kwetu tuwapeni support ya kutosha tupate katiba safi kwa maendeleo ya nchi yetu"
Atakumbukwa daima!nilimkumbuka prof Shivji na ile hotuba pale mlimani
Ni kweli ukiangalia kidini au ki-muungano hii tume haijawiana lakini tujilulize kwa niini?
Kwanza hii ni tume na sio baraza la uwakilishi; Kazi yake ni kukusanya maoni, kufanya majumuisho na kutoa pendekezo kutokana na maoni yetu tutakayoyatoa. Si lazima tukubali mapendekezo hayo. Mfano tume ya vyama vingi maoni yetu wengi yalikuwa hapana lakini wakapendekeza tuende vyama vingi jambo ambalo lilikuwa likataliwe na utawala wa wakati huo lakini Mwalimu akatumia busara ikabidi wakubaliane nae.
Kwa misingi hiyo uwiano hapa si mahali pake
Pili: Swala la Muungano na uwiano Ni vizuri tukazingatia kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili na si watu 9 na mmoja hivyo maamuzi ya kimuungano hayazingatii ukubwa wa nchi wala idadi ya watu bali ni nchi na kila upande una haki sawa. Ila swala kuu hapa ni kuwa Muungano wetu una mapungufu mengi ambayo ndio yanayotakiwa yaangaliwe kwa uwazi ili tuweze kuwa na muungano unaozingatia tofauti na mfanano wetu mambo ambayo hayakuzingatiwa wakati wa kuweka muungano huu pengine kutokana na mazingira ya wakati ule.
Swala La Uwiano ni la muhimu sana pale tunapokuja kwenye Baraza la kutunga katiba ambalo kutokana na sheria iliyopitishwa na wenye kutawala nchi kwa leo ndio kuna mapungufu makubwa ila kwa kuwa swala la katiba ni la Maslahi vile vile na tusisahau kwamba katiba nzuri ni tishio kwa maslahi ya wanaotawala sasa hivi na hilo wanalijua fika kwa hiyo huu mpambano hautaishia hapa Mwanakijiji amepambanua vizuri sana kuhusu mapungufu yaliyoko kwenye Baraza hili na kwa kweli ukiliangalia ni kuwa hii kwa kiasi kikubwa itakuwa katiba ya Chama na si ya watu. Na pia sijaona kama swala la Muungano linaguswa vipi maana kutokuliangalia kwa mapana yake ni kuendeleza ugonjwa..
Sasa nini jukumu letu sisi tunaoelewa fika kuwa mchakato huu una mapungufu makubwa na ni wazi mwisho wake katiba itakayopatikana itakuwa na mapungufu. Wajibu wetu ni kujitokeza kwa wingi, kujenga umoja na kuweka msukumo mkubwa wa tume kuhakikisha maoni yanakusanywa kwa uhakika. Vile vile kutakuwa na haja ya kuweka msukumo mkubwa kwenye baraza na baadae tutapima Kama katiba itakayopendekezwa ni bora kiasi gani kuliko hii ya sasa na kama ikionekana ni ubabaishaji ndio tutapima nguvu mbadala kwenye kura ya maoni kwa kuipinga kama ODM walivyofanya Kenya.
Lakini nasisitiza nguvu ya kimasilahi ya wanaofaidika na katiba ya sasa ni kubwa hivyo mpambano huu ni mrefu na ninaamini hata hiyo katiba ikipita kesho yake tutaendelea kudai katiba ya kweli ya wananchi.
Hayo ndio maoni yangu kwa kuwa siamini kupinga kwa maana ya kupinga tu ni tija kama hatutajiuliza tutapinga vipi na tupime matokeo ya kupinga huko. Kwa kifupi Tupinge kwa kushiriki kikamilifu.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake na utujalie muamko wa kutumia fikra zetu kwa manufaa ya nchi yetu!