Tume ya kuchunguza matokeo ya mitihani ni sahihi

Tume ya kuchunguza matokeo ya mitihani ni sahihi

mwenendo

Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
11
Reaction score
2
TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA MITIHANI NI SAHIHI
Taarifa kwa ufupi ya Tume ya kuchunguza matokeo ya mitihani iliyoteuliwa na Mh. Pinda, inaporipoti kuwa mitihani ilikuwa ni madudu na ilitayarishwa na watu wasio na sifa ni sahihi. Baadhi ya maprofesa waliojitokeza kuipinga tume hiyo, mawazo yao yako nje kabisa na jinsi tume ilivyosema.

Kila karatasi la mtihani lilikuwa na swali, “Answer the following alternative questions”. Je, “Alternative questions” ni sawa na “Multiple choice questions?” Maprofesa hao walihoji ripoti kuhusu ugumu wa mitihani kulinganisha na nchi nyingine. Maswali hayo wangeuliza tume ilibaini vipi taarifa hiyo ndipo waongee magazetini.

Je, mbona hawahoji taarifa inayosema kuwa katika karatasi la Hisabati, mwanafunzi alipata alama 12 kwa swali ambalo halipo kwenye mtihani? Wakumbuke kuwa maswali yaliyochambuliwa ni sampuli ndogo tu.

Ni kweli kabisa kuwa kama profesa alitunga mtihani na hana taaluma ya ualimu, huyu hana sifa za kutunga mitihani wala kuisanifu.

Wizara inatakiwa kupendekeza watu kwa kazi hiyo au kutoa mwongozo wake.
 
Elimu yetu magumashi matupu kuanzia waziri, manaibu wake hadi katibu mkuu WA baraza wote Ni changamoto
 
Back
Top Bottom