Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yawataja wabunge 18 waliopita bila kupingwa. Wamo Nape, Kigwangala, January, Kabudi, Mnyeti...

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
1. Ushetu - Elias Kwandikwa
2. Kongwa - Job Ndugai
3. Gairo - Ahmed Shabiby
4. Kilosa - Palamagamba Kabudi
5. Mvomero - Jonas Van Zeeland
6. Morogoro Kusini - Kalogereris Innocent
7. Morogoro Mashariki - Taletale Hamis Shabani
8. Mlele - Eng. Isaack Kamwelwe
9. Kavuu - Geofrey Pinda
10. Songwe - Philipo Mulugo
11. Bukene - Zedi Jumanne
12. Nzega Vijijini - Hamis Kigwangalla
13. Ruangwa - Kassim Majaliwa
14. Mtama - Nape Nnauye
15. Namtumbo - Vita Kawawa


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dk.Wilson Mahera (katikati) akizunghumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Tume Njendengwa Jijini Dodoma leo ambapo ametangaza majimbo 18 ya uchaguzi ambayo wagombea wake wamepita bila kupingwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpigakura, Givness Aswile na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Habari na Elimu ya Mpigakura, Dk. Cosmas Mwaisobwa.

======

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUTEULIWA WAGOMBEA PEKEE WA UBUNGE KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2020 #uchaguzimkuu2020
 
Namwona mzee wa dawa ya Madagascar ameoneshwa njia na JPM.. Sasa ni mwendo wa kutusua tu
 
Yaani Magufuli katengenezea njia watu wa kumsaidia kwenye kampeni

January, Nape na kabudi mwaka huu watalala na viatu.

Lissu atawatesa Sana na kesho tunaanza maandamano kwenye Majimbo yenu hakuna Cha kupita bila kupingwa.

Mngeanza na Jiwe aliyeshindwa kujaza form ningewaelewa

Uhuni sasa basi.....
 
Vipi pressure imepanda? Mbona bado mapema?
 
Mmekwisha kabisa dalili ya kushindwa ni kutokusoma ilani ya uchaguzi kama 2015 alivyoshindwa kusoma Lowassa jangwani!
 
Utapiga kelele weee mwisho utalala.
 
Hii ilikuwa tarehe aliyopigwa risasi mdau alitoa unabii wake
 
Sioni mpinzani akitangazwa ubunge au udiwani sioni, wanaweza achwa wawili watatu kuzugia kwamba kuna upinzani ila kwa mwendo huu sioni mpinzani anaerudi bungeni.


Inabidi kitokee kitu au jambo lisilo la kawaida kubadili huu upepo na mwelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…