Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yawataja wabunge 18 waliopita bila kupingwa. Wamo Nape, Kigwangala, January, Kabudi, Mnyeti...

Dah hii ni hatar sana,inamaana wagombea wa ccm wajua zaid kujaza fomu ya uchaguzi kuliko vyama vingine? Hii hujuma hata mpumbavu anajua tu kuwa kunamchezo umechezwa
Wew sio kila kitu ni form wengine wameamua kuuza jimbo kwa kufanya vituko ili waonekane kuan shida mwingine kuchukua form warudishe wakati ofisi imefungwa
 
yaani waliopita ni MACCM tu.hakuna mpinzani aliyepita bila kupingea ,kweli shetani humsaidia shetani mwenzie ,NEC ni CCM pure
 
Kweli mkuu
 
Lijuakali "jinsi tulivyoiba kura..."
Lowassa pamoja na uzito wake wa kushindwa kujieleza jukwaani aliweza kupata kura nyingi kumzidi Magufuli.

Baada ya tume kupindua matokeo ndipo jamaa yenu akatangazwa mshindi,mwaka huu mnalo.
 
Leta picha tu za hayo maandamano
 
Chama cha Demokrasia Bandia
 
Tume hii sio guru na imejidhihirisha ilivyojibu pingamizi la lissu dhidi ya rais magufuli na prof lipumba, ule uamuzi sio wa kisheria.
Pili,kutosikiliza rufaa za wabunge wa upinzani kwa weledi,
Hapa wanazidisha fitina tu kwa wapinzani wakihisi Cdm,act watajitoa ndiyo wanachohisi
 
Hawa nao hawana tofauti na TBC!!

Watu waliofoji vyeti vya shule/degree zao, unategemea watapenda kufanya haki kwenye uchaguzi? Kuna vitu tunatakiwa kujifunza tu kwa kuangalia watu na asili zao.
 
Hii kupita bila kupingwa si ndio iliyowaletea matatizo Clouds!??
 
Lowassa pamoja na uzito wake wa kushindwa kujieleza jukwaani aliweza kupata kura nyingi kumzidi Magufuli.

Baada ya tume kupindua matokeo ndipo jamaa yenu akatangazwa mshindi,mwaka huu mnalo.
Nini kinazuia kupindua matokeo mwaka huu??
 
Kiukweli EL aliitikisa ngome ya CCM 2015 ilihitajika kazi ya ziada
Baada ya uchaguzi huu upinzani unaenda kusahaulika Tanzania
Na hapa ndio tutamuelewa John Pombe Magufuli na ile kauli mbiu yake ya HAPA KAZI TUU
 
Sheria za Uchaguzi zinasema, baada ya uchaguzi mtu mwenye rufaa dhidi ya uteuzi au ambaye hajaridhika na mwenendo wa uchaguzi au ambaye hajaridhika na matokeo ya uchaguzi, atatakiwa kufungua kesi mahamakamani kupinga uchaguzi huo. Huu ndio muda wa kufanya hivyo katika hayo majimbo kwa maana tayari uchaguzi umefanyika.

Muda huu ni mzuri maana hata wanasheria wa serikali na TUME watashindwa kujigawa kwa kuwa kwenye uchaguzi wa majimbo mengine kupika matokeo na kuhudhuria mahakamani kuendesha kesi hizi zilizofunguliwa tayari.

Na kwa kuwa mahakama nayo kwa sasa ni kama imekuwa ya 'serikali' ni vyema kufanya muda huu ili kutoa picha ya kesi za uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba 2020 zitakuwaje, kesi hizi za sasa zitasaidia kujua kama mahakama itakuwa impartial au la.

Jibu la impartiality ya mahakama litapelekea jibu la jambo lingine ambalo ndio pekee la kuleta mabadiliko hapa nchini, tunalosubiri kutoka mdomoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani
 
Yule dogo wa CDM Bukene imekuwaje Zedi kapita bila kupingwa?
 
Je waliokatwa wanafursa ya kwenda kusimamisha uchaguzi katika majimbo yao hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa ?.

Je Mahakama ina uwezo wa kuwarejesha wagombea wote waliokatwa ?.

Je Tume ya uchaguzi kwa mwenendo huu bado yaweza kusimamia uchaguzi huru na haki ?!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…