Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeshiriki maonyesho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yanaendelea Mkoani Kagera

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeshiriki maonyesho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yanaendelea Mkoani Kagera

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Na Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeshiriki maonyesho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yanaendelea Mkoani Kagera.

Akifungua maonyesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga amesema Mkoa wa Kagera unakabiliwa na changamoto ya udumavu hivyo amewataka wadau wa lishe wakiwemo washiriki wa maonyesho hayo kwa ujumla kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara y Uendeshaji kutoka NIRC Salome Njau amesema Tume wamejiandaa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu namna bora ya uzalishaji na majukumu ya tume kama kusimamia,kuratibu na kuendeleza miundombinu yote ya umwagiliaji nchini.

Pia amewataka wakulima mkoani Kagera na maeneo jirani kutumia fursa ya maonyesho hayo kujufaika na uwezeshaji unaofanywa na Tume kuhusu kilimo cha umagiliaji lengo ni kuwa na kilimo cha kisasa chenye tija kwa maslahi ya ndani na nje kwa kuilisha dunia.
IMG-20241016-WA0047.jpg
IMG-20241016-WA0046.jpg
IMG-20241016-WA0045.jpg
IMG-20241016-WA0044.jpg
IMG-20241016-WA0043.jpg
IMG-20241016-WA0042.jpg
IMG-20241016-WA0033.jpg
 
Pia KATERERO kuna shida ya umwagiliaji.
Wapatembelee
 
Back
Top Bottom