Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,550
Heshima kwenu wakuu.
Ni muda mrefu umepita tangu madiwani wa kata katika halmashauri mbalimbali nchini kujiuzulu udiwani na kujiunga na ccm ili 'kuunga mkono' juhudi za rais Magufuli.Aidha kuna madiwani ambao wamefariki na wengine waliokosa sifa za kuwa madiwani kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo baadaye ilikuja kugundulika madiwani hao hawakujiuzulu ili 'kuunga mkono juhudi za rais' bali walinunuliwa kwa fedha taslimu,ahadi za kulipiwa madeni pamoja na ahadi zakupewa nafasi ya kugombea tena nafasi hizo kupitia ccm na kuhakikishiwa ushindi hata kama ni kwa mtutu wa bunduki.Mradi huu wa kununua wawakilishi wa wananchi upo chini ya katibu wa halmashauri kuu ya ccm Taifa itikadi na uenezi Humphrey Polepole na bado unaendelea!
Kwa muda wote huo wananchi wa kata husika wamekosa uwakilishi kwenye mabaraza ya halmashauri hivyo kero zao kushindwa kutatuliwa na halmashauri husika kutokana na kukosa watu wa kuwasemea.Ni dhambi kubwa sana imefanywa na ccm dhidi ya wananchi kwa kuwakosesha uwakilishi kutokana na kuwarubuni wawakilishi wao ili wajiuzulu.
Awali tuliona kata au majimbo yanapokuwa wazi baada ya madiwani na wabunge husika kununuliwa tume ya uchaguzi NEC hutangaza mchakato wa uchaguzi ndani ya muda mfupi,kwa mfano Mollel na Mtulia walijiuzulu mwezi desemba 2017 na uchaguzi mdogo ukafanyika mwezi February 2018 pamoja na wa madiwani wa kata 6 waliokuwa wamejiuzulu.
Kuna tetesi kwamba tume ya uchaguzi imeshindwa kuendesha uchaguzi kwenye kata nyingi tu zilizo wazi kutokana na ukosefu wa fedha kwani wameomba fedha hazina na kujibiwa hakuna fedha kwa sasa wasubiri.Kuna madiwani walijiuzulu tangu mwezi January na wengine February lakini mpaka leo mwezi Mei uchaguzi haujafanyika.
Serikali ya ccm inapaswa kuipatia NEC fedha iendeshe uchaguzi ili wananchi wapate wawakilishi. Wakati ccm wananunua madiwani hawakujua kwamba kutakuwa na gharama za kuwapata wengine?
Kutokana na sheria za uchaguzi wa madiwani na wabunge, uchaguzi mdogo hautafanyika chini ya miaka miwili kabla ya mchakato wa uchaguzi mkuu unaofuata kuanza.Kwa kawaida mchakato wa uchaguzi mkuu huanza mwezi julai hivyo ifikapo mwezi July mwaka huu itabaki miaka miwili kabla ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2020 kuanza kwa hiyo hakutakuwa na uchaguzi mdogo tena.Hofu yangu uchaguzi usipofanyika ndani ya mwezi huu na mwezi ujao wa juni wananchi wa kata husika wanaweza kukosa uwakilishi mpaka 2020!