Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi ina 'double standards' kwenye kusimamia ratiba ya kampeni kwa wagombea

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi ina 'double standards' kwenye kusimamia ratiba ya kampeni kwa wagombea

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Ratiba rasmi ya NEC toleo la 5 la Octoba 2 mwaka huu, inaonesha namna wagombea wa vyama vyote sehemu wanazotakiwa kuwepo kwenye mikutano rasmi ya kampeni. Lakini kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa ratiba hiyo kwa upande wa CCM na mgombea wake. NEC inaonesha kuigwaya CCM na mgombea wake.

Mara kadhaa amekuwa akikiuka kufuata ratiba hiyo na NEC chini ya Mkurugenzi wake Charles Mahera hawajawahi kuonya, kukaripia wala kushauri wagombea kufuata ratiba hiyo. Na bado mgombea wa CCM anafuata ratiba yake mwenyewe. Tukianzia na tukio la kuingilia ratiba ya Chadema tarehe 18.9.2020 mjini Kigoma.

Hakupaswa awepo lakini akabakia kwa kisingizio cha majukumu ya urais. Ni wakati wanajua akiwemo mgombea wa Urais eneo fulani haiapswi mwingine kuwepo eneo hilo. Aliondoka siku ya pili yake jumapili. kafanya maandalizi ya Lissu yakwame.

Ijumaa tena 9.10.2020 hakuwa kwenye ratiba ya kampeni lakini akaitisha watu uwanja wa Taifa na kupiga kampeni pale. NEC wapo tu kimya. Ratiba inavurugwa wazi wazi lakini wao wapo kimya. Kazi yao kumtazama Lissu tu amesema nini ili wamshikishe adhabu. Double standards kwa tume hii ni kubwa sana. Wanadhani wapo kwa ajili ya CCM tu.

Mbali na hilo lakini wana kashfa za kutosha zinazotolewa kwenye majukwaa yao na wala hawasemi lolote. Polepole amekuwa kinara wa kashfa na kutoa lugha za kebehi mno. NEC ipo kimya.

Ina mwogopa sana aliyewachagua. Hii sio tume huru japo Mahera anajimwambafai kuwa haiingiliwi wala kupangiwa wala kutishwa na mtu yeyote. Watanzania tunaona hayo yanyofanyika. Tupo tunawasubiri kwenye kona ya makutano.
 
Tume huru Tume huru Tume huru Tume huru Tume huru Tume huru Tume huru ndio janga letu.
 
Hakuna taasisi huru nchi hii, Urais pekee ndio taasisi huru. Wangalau taasisi zinazojiita huru, huwa zina uhuru wa kiasi fulani tunapokuwa na rais asiye na ulevi wa madaraka. Hao wanaosema wako huru wanasema hivyo ili kupunguza hasira za wananchi, ila hata wao wanajua kabisa hakuna kitu kama hicho.

Bila kutokea machafuko na kupata katiba mpya itakayoondoa kufungu cha rais kushitakiwa akiwa au ametoka madarakani, hakuna taasisi itakuwa huru ndani ya nchi hii.
 
Hao NEC ndio wataenda kuvuruga uchaguzi kwa ujinga wao wa kujipendekeza kwa bosi wao, na lolote litakalotokea baada ya hapo wao NEC ndio wataubeba huo msalaba wao.

Watanzania sio wajinga.
 
Tatizo lenu mnajitoa ufahamu kutaka ligi na president. Fanyeni yenu achaneni kabisa na huyo mtu. Mnavyopenda ligi za kihuni hamtasikia
 
Hao NEC ndio wataenda kuvuruga uchaguzi kwa ujinga wao wa kujipendekeza kwa bosi wao, na lolote litakalotokea baada ya hapo wao NEC ndio wataubeba huo msalaba wao.

Watanzania sio wajinga.
Nawaza sana jinsi Mahera sura yake itakavyo kuwa pale The Hague huku akilazimishwa kuvaa barakoa
 
Hakuna taasisi huru nchi hii, Urais pekee ndio taasisi huru. Wangalau taasisi zinazojiita huru, huwa zina uhuru wa kiasi fulani tunapokuwa na rais asiye na ulevi wa madaraka. Hao wanaosema wako huru wanasema hivyo ili kupunguza hasira za wananchi, ila hata wao wanajua kabisa hakuna kitu kama hicho.

Bila kutokea machafuko na kupata katiba mpya itakayoondoa kufungu cha rais kushitakiwa akiwa au ametoka madarakani, hakuna taasisi itakuwa huru ndani ya nchi hii.


Ni kweli kabisa kama tutakua na Rais anayeweza kufanya chochote na asiaulizwe zaidi ya kusifiwa na kutukuzwa mpaka na viongozi wa Dini huku wakimwita mtu aliyetaka kuuawa kuwa ni msaliti na anataka kuuza nchi, tutakua tunakaribisha vurugu tu na si vinginevyo. Tumeshindwa kutofautisha nchi na CCM.

Tuwaase wapinzani hasa ACT Wazalendo na Chadema wiki moja ya mwisho wahamasishe wapiga kura wao wafanye dua na kuomba sana kwa Mungu ili wale wote watakaovuruga Kura waanguke mbele ya mkono wa Mwenyezi Mungu. Mungu ndiye pekee anayeweza kuwaondoa madhalimu kwa wakati.
 
Huyo charles mahera ni robot tu fikiria a PHD holder anaendeshwa na polepole lakini akae akijuwa yeye ni chambo tu 28. November 2020 ndio mwisho wa ngebe zake
 
Hili zee limeshavurugwa! Hatuna muda wa kupeleka taahira kwenye jengo letu!
 
Ratiba rasmi ya NEC toleo la 5 la Octoba 2 mwaka huu, inaonesha namna wagombea wa vyama vyote sehemu wanazotakiwa kuwepo kwenye mikutano rasmi ya kampeni. Lakini kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa ratiba hiyo kwa upande wa CCM na mgombea wake. NEC inaonesha kuigwaya CCM na mgombea wake...
Hakuna kinachoniudhi mimi kama kauli ya 'slow slow' - eti 'Chama cha Mbowe' TENA akiwa katika mikutano rasmi! Hii ni dharau kwa taasisi kubwa kama CHADEMA, ni dharau kwa mfumo wa Vyama vingi na Bunge pamoja na Serikali ambao wanakitambua Chama CHADEMA na kamwe hawajatoa fedha au matamko kama ya huyu Slow slow!
 
Back
Top Bottom