Pre GE2025 Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, Itakuwa Huru Kweli au ni Jina tu? Ukiomba Mambo 10 Ukapewa 1, Shukuru kwa Hilo 1. Asante kwa INEC!

Pre GE2025 Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, Itakuwa Huru Kweli au ni Jina tu? Ukiomba Mambo 10 Ukapewa 1, Shukuru kwa Hilo 1. Asante kwa INEC!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kulihitajika mabadiliko madogo ya katiba kabla ya mabadiliko ya sheria. Hakuna faida ya kutoheshimisha katiba. Katiba ipewe Hadji yake ya kuwa supreme over anything ndani ya nchi. Katiba iogopwe. Katiba haiwezi kujitetea. Inatakiwa itetewe. Katiba itajitetea kwa nchi kuharibika na kila mtu kujiendea. Kilichomsaida Mabeyo na wenzake 2021 kuamua uelekeo wa nchi na kuleta utulivu ni katiba. Katiba ndiyo muongozo mkuu.
Wanabodi
Haya ni mapendekezo yangu kwa miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi, Sheria ya vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi.

View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=lqufL6e34DyB2Gjr
Nilipendekeza
1. Sheria yetu ya uchaguzi tunayoitunga, ifuate katiba ya JMT ibara ya 5 na Ibara ya 21.
2. Ibara ya 5 ni Haki ya kila Mtanzania kuwa huru kumchagua kiongozi anayemtaka.
3. Ibara ya 21 ni Haki ya kila Mtanzania kuwa huru kugombea na kuchaguliwa kuwa kiongozi.
4. Tufanye mabadiliko madogo ya katiba kuondoa ubatili kwenye ibara ya 39 na 67, uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.
5. Turudishe haki za Mtanzania zilizoporwa za kuchagua na kuchaguliwa.
6. Tume ya uchaguzi iitwe Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi
7. Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ufanyike siku moja.
8. Chaguzi zote mbili zisimamiwe na Tume moja Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
9. Uongozi wa vyama vya siasa, sio ajira!, ni uongozi wa kujitolea, viongozi wa vyama vya siasa hawapaswi kulipwa mishahara, ni posho tuu!.
10. Tuifute ruzuku kwa Vyama vya Siasa na badala yake tutoe ruzuku kwa yatima, wajane, wazee, wasiojoweza na wenye ulemavu.

Leo serikali imetoa taarifa ya kukubalika rasmi pendekezo moja View attachment 2959888

Japo mapendekezo yangu mengine yote yamekataliwa, ukiomba mambo 10, mambo 9 yakakataliwa, jambo moja likakubaliwa, hatua ya kwanza ni kushukuru na kupongeza kwa hilo moja lililokubaliwa, halafu uendelee kupigania yale 9 yaliyobakia yaliyo kataliwa.

Pongezi serikali yetu sikivu kubadili jina la Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi. Naomba sana lisiwe ni jina tuu, lakini mambo yakawa ni yale yale!, sote tumeshuhudia kilichotokea Zanzibar ile 2015, ZEC ni Tume huru na Shirikishi lakini kilichotokea... Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Hivyo naipongeza sana serikali yetu sikivu kukubali kubadili jina la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, swali kama Itakuwa Huru Kweli au ni Jina Tuu bado lipo mpaka tuushuhudie huo uhuru!. Ukiomba Mambo 10 Ukapewa 1, Shukuru kwa Hilo 1. Asante sana serikali yetu kwa INEC!. Yale 9 yaliyobakia, kazi inaendelea na ikibidi, kuna watu watabisha hodi mahakamani!.

Nimalizie kwa kuendelea kusisitiza Watanzania tuwe ni watu wa shukrani, tushukuru kwa madogo ili tuweze kujaaliwa makubwa!.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Rejea za Mwandishi Kuhusu Sheria Hizi.
 
Tatizo lipo ikiwezekana tunapiga kura tupige live kama nchi za wenzetu ijapokuwa kutakuja hoja kwamba hatuna uwezo wa hiyo technology lakini ikumbukwe hapo watu wanapigania haki zao za msingi baada ya kukosa Imani na utaratibu uliopo
 
Back
Top Bottom