Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi makali kama msumeno

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Ninaandika haya Mungu bariki hatimaye tume wakajue kuna watu tumefunga tunawaombea wao kwa Mungu ili wakapate kutenda haki. Yaani wao kama nchumeno wakakate kwa mbele na kwa nyuma pia.

Kwa upande wetu wana maombi, tunaiona hatari inayotunyemelea sisi kama taifa iwapo tume itaamua nayo kuendekeza nyimbo za waliojinasibu kuwa wao ndiyo waliowateua. Kuwa eti kwa sababu hiyo hawana ruksa ya kuwatangaza wasiowataka wao kama washindi.

Tamko la leo kuhusiana na wanaosemekana kuwa wanatukana badala ya kusema sera zao limetustua wanamaombi sisi, kiasi tukadhani tusisubiri tu majibu ya maombi yetu kuwafikia wao tume kiitifaki kutokea kwa Mungu.

Hoja za kuwa pana matusi zimekuwa zikitolewa na chama kimojawapo katika vinavyoshindana na kwa muda mrefu sasa. Hii ikiwa hata kabla mno ya kampeni. Shutuma hizi zimeendelea kuwapo bila ya kuwepo au kutolewa ushahidi wowote wa matusi hayo. Kiasi sasa wimbo huu tulikuwa tunaanza kuuzoea kuwa ni moja katika harakati za mfa maji kwenye mpambano ulio mgumu vilivyo.

Kwamba tume nao wanaanza kuimba nyimbo hizi? Tunaomba ushahidi tafadhali wa matusi hayo neno kwa neno na mantiki kwa mantiki.

Vinginevyo kututumbukiza kwenye mtego wa maafisa uteuzi kwaweza kusituache salama. Tume kama waamuzi itakuwa hatari kubwa kuonekana kujipanga upande wa baina ya washindani wowote.

Tume nyie kama msumeno kataji yenu ikianza kuwa na macho mbona itakuwa kutelekeza wajibu wenu na hata kuuimarisha vilivyo uhitaji wa tume iliyo huru na kwa hali ya dharura mno?

Kwamba pana wagombea wameenguliwa nao wanalalimikia enguaji hizo. Kwamba muda wa kampeni unazidi kuyoyoma hali washindani wao wakichanja mbuga? Tume warejesheni Wagombea hao kwenye sanduku la kura wananchi wakaamue wenyewe. Hebu msiishiriki laana ya kuwatendea wengine dhuluma.

Msiwanyime haki na uhuru wao wagombea hawa na hata wapiga kura, mkiridhia matakwa ya washindani fulani. Kila mtu na akajishindie mechi zake bila ya kuwashinikiza nyie (au nyie kujipendekeza) kwa usaidizi spesheli.

Macho yetu kodo, Ruangwa, Kilosa, Mtama, Ushetu na kote kwenye hizi pitaji pitaji bila pingwaji.

Pamoja na yote haitakuwa sawa kutokufikishieni ombi letu jingine tulilolipeleka kwa mola pia kukuhusuni nyie. Kemeeni matumizi ya lugha za kienyeji yaliyo kinyume na kanuni zenu kwa baadhi ya wagombea. Kemeeni kauli hizi za kikabila ambapo nyingi hata zinaambatana na vitisho, rushwa na hata uchochezi nyuma ya pazia.

Kauli hizi ni za vitisho (msiponichagulia fulani hampati barabara, maji, zahanati nk). Kauli hizi zina vionjo vya rushwa (mkinichagulia fulani nami nitawaletea pia daraja, barabara Ila kama hamtaki msimchague muone nk).

Kauli hizi ni za kichochezi (fulani na fulani wanatumiwa na mabeberu, fulani na fulani wametumwa na mabeberu, fulani na fulani ni wapinga maendeleo ya watanzania, fulani na fulani ni wasaliti, fulani na fulani si wenzetu nk).

Tunapotazamia haki kutoka kwenu itapendeza kuiona haki ikitendeka hatua kwa hatua na kwa mujibu wa sheria.

Nchumeno na ukakate kwa mbele na kwa nyuma pia.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Ninawasilisha.
 
Kelele za NEC ni kama za debe tupu. Kama wanamaanisha wanachokisema waanze na Heri James...mwenyekiti wa UVCCM.

Uwepo kwa tume iliyo huru ilikuwa jambo la msingi sana. Ndiyo maana hata ndani ya nusu shari na aungwe mkono huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Kwa hakika ndiye aliye mkombozi mwema wa taifa hili.
 
Mfa maji huyo hakupenda ushindani bahati mbaya Tanzania sivyo alivyodhani.

Tumkatae mijini na vijijini sababu ni donda baya kwetu sisi wapenda haki, uhuru na maendeleo
 
Alhaj Abdullah Bulembo akimnadi jiwe kujipembejea teuzi, bungeni aliwahi pendekeza (passionately) kusiwepo uchaguzi wa rais 2020 kwa kile alichokiita jiwe akakubalika mno na hamna namna.

Kwamba eti jiwe apite bila kupingwa. Yale ya Ruangwa, kilosa, Mtama, ushetu, nk.

Sina hakika kama yungali na msimamo huo huo hii leo. Wote wamesambaratika. Jiwe anavyolia lia kuomba mitano mingine mbona anatia huruma?

Kwa dhati kabisa analia "jamani nipeni na mimi hii mitano mingine mbona wenzangu wote mliwapa? Jamani ninawasilisha itakuwa ya mwisho kabisa wala sitaongeza mingine."

Anatia huruma kuliko mgombea mwingine yeyote aliyewahi pita katika historia yetu.
 
Ni wapumbavu hawa watawala wa ccm we acha tu
 
Tume imerusha jiwe gizani chadema ndo mnalia kwa uchungu naona jiwe limewapata kisawasawa. Kwani mmetajwa kuwa nyie ndo wenye mitusi??!
 
Mfa maji huyo hakupenda ushindani bahati mbaya Tanzania sivyo alivyodhani.

Tumkatae mijini na vijijini sababu ni donda baya kwetu sisi wapenda haki, uhuru na maendeleo
Sisi tutamchagua Magufuli tena. Chadema mtaona kila rangi mwaka huu.
 
Alhaj Abdullah Bulembo akimnadi jiwe kujipembejea teuzi, bungeni aliwahi pendekeza (passionately) kusiwepo uchaguzi wa rais 2020 kwa kile alichokiita jiwe akakubalika mno na hamna namna.

Kwamba eti jiwe apite bila kupingwa. Yale ya Ruangwa, kilosa, Mtama, ushetu, nk.

Sina hakika kama yungali na msimamo huo huo hii leo. Wote wamesambaratika. Jiwe anavyolia lia kuomba mitano mingine mbona anatia huruma?

Kwa dhati kabisa analia "jamani nipeni na mimi hii mitano mingine mbona wenzangu wote mliwapa? Jamani ninawasilisha itakuwa ya mwisho kabisa wala sitaongeza mingine."

Anatia huruma kuliko mgombea mwingine yeyote aliyewahi pita katika historia yetu.
Magufuli bado ni chaguo la watanzania. Chadema mtaongea sana mwaka huu.
 
Tume imerusha jiwe gizani chadema ndo mnalia kwa uchungu naona jiwe limewapata kisawasawa. Kwani mmetajwa kuwa nyie ndo wenye mitusi??!

Kwani kuna ametajwa? Au nyie ni hawa wa lugha za kienyeji zenye vilivyo jificha nyuma ya pazia?

Au nyie ndiyo msiotaka watangaze walio washindi kisa mliwateua nyie?

Hampendi tume kujikita kwenye haki?

Manyang'alu wakubwa nyie!
 
Magufuli bado ni chaguo la watanzania. Chadema mtaongea sana mwaka huu.

Tupo watanzania wengi tu ambao huyu bwana si chaguzi letu.

Tume ikitenda mambo kwa uhuru na haki huyu bwana hakatizi kwenye sanduku la kura.
 
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Ninaandika haya Mungu bariki hatimaye tume wakajue kuna watu tumefunga tunawaombea wao kwa Mungu ili wakapate kutenda haki. Yaani wao kama nchumeno wakakate kwa mbele na kwa nyuma pia.

Kwa upande wetu wana maombi, tunaiona hatari inayotunyemelea sisi kama taifa iwapo tume itaamua nayo kuendekeza nyimbo za waliojinasibu kuwa wao ndiyo waliowateua. Kuwa eti kwa sababu hiyo hawana ruksa ya kuwatangaza wasiowataka wao kama washindi.

Tamko la leo kuhusiana na wanaosemekana kuwa wanatukana badala ya kusema sera zao limetustua wanamaombi sisi, kiasi tukadhani tusisubiri tu majibu ya maombi yetu kuwafikia wao tume kiitifaki kutokea kwa Mungu.

Hoja za kuwa pana matusi zimekuwa zikitolewa na chama kimojawapo katika vinavyoshindana na kwa muda mrefu sasa. Hii ikiwa hata kabla mno ya kampeni. Shutuma hizi zimeendelea kuwapo bila ya kuwepo au kutolewa ushahidi wowote wa matusi hayo. Kiasi sasa wimbo huu tulikuwa tunaanza kuuzoea kuwa ni moja katika harakati za mfa maji kwenye mpambano ulio mgumu vilivyo.

Kwamba tume nao wanaanza kuimba nyimbo hizi? Tunaomba ushahidi tafadhali wa matusi hayo neno kwa neno na mantiki kwa mantiki.

Vinginevyo kututumbukiza kwenye mtego wa maafisa uteuzi kwaweza kusituache salama. Tume kama waamuzi itakuwa hatari kubwa kuonekana kujipanga upande wa baina ya washindani wowote.

Tume nyie kama msumeno kataji yenu ikianza kuwa na macho mbona itakuwa kutelekeza wajibu wenu na hata kuuimarisha vilivyo uhitaji wa tume iliyo huru na kwa hali ya dharura mno?

Kwamba pana wagombea wameenguliwa nao wanalalimikia enguaji hizo. Kwamba muda wa kampeni unazidi kuyoyoma hali washindani wao wakichanja mbuga? Tume warejesheni Wagombea hao kwenye sanduku la kura wananchi wakaamue wenyewe. Hebu msiishiriki laana ya kuwatendea wengine dhuluma.

Msiwanyime haki na uhuru wao wagombea hawa na hata wapiga kura, mkiridhia matakwa ya washindani fulani. Kila mtu na akajishindie mechi zake bila ya kuwashinikiza nyie (au nyie kujipendekeza) kwa usaidizi spesheli.

Macho yetu kodo, Ruangwa, Kilosa, Mtama, Ushetu na kote kwenye hizi pitaji pitaji bila pingwaji.

Pamoja na yote haitakuwa sawa kutokufikishieni ombi letu jingine tulilolipeleka kwa mola pia kukuhusuni nyie. Kemeeni matumizi ya lugha za kienyeji yaliyo kinyume na kanuni zenu kwa baadhi ya wagombea. Kemeeni kauli hizi za kikabila ambapo nyingi hata zinaambatana na vitisho, rushwa na hata uchochezi nyuma ya pazia.

Kauli hizi ni za vitisho (msiponichagulia fulani hampati barabara, maji, zahanati nk). Kauli hizi zina vionjo vya rushwa (mkinichagulia fulani nami nitawaletea pia daraja, barabara Ila kama hamtaki msimchague muone nk).

Kauli hizi ni za kichochezi (fulani na fulani wanatumiwa na mabeberu, fulani na fulani wametumwa na mabeberu, fulani na fulani ni wapinga maendeleo ya watanzania, fulani na fulani ni wasaliti, fulani na fulani si wenzetu nk).

Tunapotazamia haki kutoka kwenu itapendeza kuiona haki ikitendeka hatua kwa hatua na kwa mujibu wa sheria.

Nchumeno na ukakate kwa mbele na kwa nyuma pia.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Ninawasilisha.
NEC imejaa wapuuzi ile.

Watu wasio na utu hata kidogo.

Ni watu wazima lakini akili zao hazina tofauti na watoto wadogo.

Tume ya uchaguzi ndiyo inayoshiriki kuhujumu uchaguzi
 
Kwani kuna ametajwa? Au nyie ni hawa wa lugha za kienyeji zenye vilivyo jificha nyuma ya pazia?

Au nyie ndiyo msiotaka watangaze walio washindi kisa mliwateua nyie?

Hampendi tume kujikita kwenye haki?

Manyang'alu wakubwa nyie!
mpaka dakika hii ni chadema tu ndo wanalia kwanini tume imekataza matusi kwenye kampeni? Comrade mlitakaje? Muendelee tu kutukana?
 
Back
Top Bottom