Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Ninaandika haya Mungu bariki hatimaye tume wakajue kuna watu tumefunga tunawaombea wao kwa Mungu ili wakapate kutenda haki. Yaani wao kama nchumeno wakakate kwa mbele na kwa nyuma pia.
Kwa upande wetu wana maombi, tunaiona hatari inayotunyemelea sisi kama taifa iwapo tume itaamua nayo kuendekeza nyimbo za waliojinasibu kuwa wao ndiyo waliowateua. Kuwa eti kwa sababu hiyo hawana ruksa ya kuwatangaza wasiowataka wao kama washindi.
Tamko la leo kuhusiana na wanaosemekana kuwa wanatukana badala ya kusema sera zao limetustua wanamaombi sisi, kiasi tukadhani tusisubiri tu majibu ya maombi yetu kuwafikia wao tume kiitifaki kutokea kwa Mungu.
Hoja za kuwa pana matusi zimekuwa zikitolewa na chama kimojawapo katika vinavyoshindana na kwa muda mrefu sasa. Hii ikiwa hata kabla mno ya kampeni. Shutuma hizi zimeendelea kuwapo bila ya kuwepo au kutolewa ushahidi wowote wa matusi hayo. Kiasi sasa wimbo huu tulikuwa tunaanza kuuzoea kuwa ni moja katika harakati za mfa maji kwenye mpambano ulio mgumu vilivyo.
Kwamba tume nao wanaanza kuimba nyimbo hizi? Tunaomba ushahidi tafadhali wa matusi hayo neno kwa neno na mantiki kwa mantiki.
Vinginevyo kututumbukiza kwenye mtego wa maafisa uteuzi kwaweza kusituache salama. Tume kama waamuzi itakuwa hatari kubwa kuonekana kujipanga upande wa baina ya washindani wowote.
Tume nyie kama msumeno kataji yenu ikianza kuwa na macho mbona itakuwa kutelekeza wajibu wenu na hata kuuimarisha vilivyo uhitaji wa tume iliyo huru na kwa hali ya dharura mno?
Kwamba pana wagombea wameenguliwa nao wanalalimikia enguaji hizo. Kwamba muda wa kampeni unazidi kuyoyoma hali washindani wao wakichanja mbuga? Tume warejesheni Wagombea hao kwenye sanduku la kura wananchi wakaamue wenyewe. Hebu msiishiriki laana ya kuwatendea wengine dhuluma.
Msiwanyime haki na uhuru wao wagombea hawa na hata wapiga kura, mkiridhia matakwa ya washindani fulani. Kila mtu na akajishindie mechi zake bila ya kuwashinikiza nyie (au nyie kujipendekeza) kwa usaidizi spesheli.
Macho yetu kodo, Ruangwa, Kilosa, Mtama, Ushetu na kote kwenye hizi pitaji pitaji bila pingwaji.
Pamoja na yote haitakuwa sawa kutokufikishieni ombi letu jingine tulilolipeleka kwa mola pia kukuhusuni nyie. Kemeeni matumizi ya lugha za kienyeji yaliyo kinyume na kanuni zenu kwa baadhi ya wagombea. Kemeeni kauli hizi za kikabila ambapo nyingi hata zinaambatana na vitisho, rushwa na hata uchochezi nyuma ya pazia.
Kauli hizi ni za vitisho (msiponichagulia fulani hampati barabara, maji, zahanati nk). Kauli hizi zina vionjo vya rushwa (mkinichagulia fulani nami nitawaletea pia daraja, barabara Ila kama hamtaki msimchague muone nk).
Kauli hizi ni za kichochezi (fulani na fulani wanatumiwa na mabeberu, fulani na fulani wametumwa na mabeberu, fulani na fulani ni wapinga maendeleo ya watanzania, fulani na fulani ni wasaliti, fulani na fulani si wenzetu nk).
Tunapotazamia haki kutoka kwenu itapendeza kuiona haki ikitendeka hatua kwa hatua na kwa mujibu wa sheria.
Nchumeno na ukakate kwa mbele na kwa nyuma pia.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Ninawasilisha.