Comrade kuna sheria zinazosimamia zoezi zima la uchaguzi. Wagombea walioenguliwa wameenguliwa kwa sababu mbalimbali na sio wameonewa. Kutakua na tija gani ya kutunga sheria halafu tusizitumie?
Kwa mfano Wakati Lissu ameweka mapingamizi dhidi ya Magufuli, lengo lake lilikuwa ni kuishawishi tume imuengue Magufuli. Na kama sababu za Lissu zingekua na tija Magufuli angeenguliwa na tume. Lingetokea hilo sidhani kama chadema mngekuja hapa kusisitiza Magufuli arudishwe kwenye kinyang'anyiro.
Mkuu kinadharia ulichoandika kinaweza onekana kuwa ni sawa lakini kiuhalisia sivyo.
Lissu aliweka mapingamizi yale kwa kuamini kutakuwa na mapingamizi dhidi yake tokea CCM na tokea CUF. Ndiyo maana alisema tangia mapema kabisa asienguliwe mtu yeyote mezani. Twende kwa wapiga kura, kwenye sanduku la kura.
Lissu hakuwa na nia ya kumwengua JPM wala Lipumba. Wala CDM wasingeshabikia enguaji yoyote.
Sababu nyingi za mapingamizi haya hazina mashiko. Kwa utangamano wa nchi rejesha wote wanaolalamika. Kumbuka hakuna engua engua yoyote iliwahi pita tangia nchi hii kupata uhuru isipokuwa wakati wa awamu ya 5. Haikufikirishi tu?
Pia, haikufikirishi kuona kuwa wanaoenguliwa ni wapinzani tu?
Hapa ilihitaji busara zaidi kuliko taratibu fyongo zinazolalamikiwa ambazo pia zinalazimishwa kuwaengua wengine. Kumbuka taratibu hizo pia ni subject ya malalamiko kama ilivyo kutokuwapo kwa tume ya uchaguzi iliyo huru.
Majimbo ya muhimu kuonyesha nia njema ni yale ya Lindi, kilosa, kongwa na ushetu japo kuwarejesha wote kabisa wanaolalamika ni hitajio la msingi kabisa.
Busara haiwezi kushindwa na taratibu zozote zilizopo. Kumbuka hata mapingamizi ya JPM, Lipumba na hata Maalim ni busara zaidi zilizotumika kuyatupa na hapa tuko vizuri tunaendelea kwa amani.
Nikudokeze kama hujui kuridhia kuwapitisha wagombea wote kutaipa tume kuaminika zaidi katika kusonga mbele kwetu ndani ya changamoto zilizopo.
Hudhani kuna faida mno kwa tume na mstakabala wetu mzima kama taifa kwa kuwarudisha wote walioenguliwa wanaolalamika kuliko faida za kuwakomalia ili kuwaengua tu?