Uchaguzi 2020 Tume ya uchaguzi na CCM wainajisi katiba, Deo Mwanyika hastahili kuteuliwa wala kugombea ubunge kwa sababu ya kesi ya kukwepa kodi

Labda tujue kwanza tafsiri na maana ya kisheria ya;

"...Ndani ya miaka mitano asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la ukwepaji kodi...."

Sasa, sisi tunasema " amekosa sifa kwa kuwa alitiwa hatiani kwa kosa la kutolipa kodi"

Lakini, mahakama haikumtia hatiani. Kilichofanyika ni mshtakiwa na mshtaki kuelewana nje ya mahakama na kisha anayeshtaki kupeleka kusudio la "kutoendelea na kesi"...

Katika mazingira haya, hakuna hukumu ya mahakama hapa. Japo ni kweli kabisa kuwa alishtakiwa....

Lakini kabla kesi kusikilizwa hadi mwisho kisha hukumu kutolewa, ikawa imefutwa...!

Katika mazingira haya mtu atawezaje kusema alishtakiwa na kuhukumiwa na kisha amwekee pingamizi?

Kisheria, Deo Mwanyika hajawahi kuhukumiwa na mahakama kwa kosa hili...!

NEC watakuuliza swali dogo na rahisi tu, kuwa, uayo nakala ya hukumu hiyo kama ushahidi?

Hapa Deo Mwanyika kama Deo Mwanyika, hana kesi na hajawahi kuhukumiwa na mahakama kwa kosa hili...!

Shida inakuja kwa CCM kilichomteua awe mgombea wao huku kikitambua kuwa aliwahi kufanya kosa la kimaadili la kukwepa kulipa kodi na mwisho wa siku wajaelewana nje ya mahakama na akawalipa. Hili watu wote wanajua na waliona...!!

CC: Majota Cossata
 
Hiyo ya mwisho hapo chini ni uongo na upumbavu wa hali ya juu. Katiba ya JMT haisemi hivyo hata kidogo.
 
Sharia zipo kwa ajili ya upinzani kaka,hazimhusu kila mtu, elewa hilo
 
Hatari sana nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…