Tume ya Uchaguzi(NEC), yapendekeza Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuleta ufanisi

Tume ya Uchaguzi(NEC), yapendekeza Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuleta ufanisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Tume ya Taifa ya UCHAGUZI (NEC) inapendekeza yafuatayo:-

1. Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuongeza ufanisi.

2. Tume iwe na watumishi wake mpaka ngazi ya Wilaya.

3. Kuwe na sheria moja ya Uchaguzi.

4. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume.

5. Wanaopita bila kupingwa Wabunge na Madiwani wapigiwe kura za NDIYO/ HAPANA.

6. Asasi zinazotoa elimu ya Uraia ziwezeshwe na Serikali.

=====

NEC YATOA MAPENDEKEZO 5 KUJIENDESHA KIUFANISI

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa mapendekezo matano kwa serikali kutaka itungwe Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakayoiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Mwenyekiti wa NEC , Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage alitoa mapendekezo hayo kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwasilisha taarifa Taarifa ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020 Ikulu Dar es Salaam jana.

Alisema tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, iliendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kwa pamoja walitoa mapendekezo hayo waliyoyawasilisha kwa Rais.

Aliyataja mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na kutungwa kwa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itaiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Mapendekezo mengine ni kuwepo na watendaji wa Tume hadi ngazi ya halmashauri, mamlaka husika ziangalie uwezekano wa kuunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 ili kurahisisha utekelezaji wa sheria hizo.

Pia Tume ilipendekeza kuwa sheria za uchaguzi zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili pamoja na serikali kuangalia uwezekano wa kuziwezesha kifedha asasi na taasisi zinazotoa elimu ya mpiga kura katika hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.

Akijibu kuhusu mapendekezo hayo, Rais Samia alisema yote ni ya msingi na jambo muhimu ni kwa wadau kuyajadili kwa kina na kupeleka mapendekezo yao serikalini ili ione namna itakavyoweza kuyafanyia kazi.

Hata hivyo, Samia alisema changamoto aliyoiona ni pale serikali ilipotakiwa kuwa na wasimamizi wa kudumu wa uchaguzi mpaka ngazi ya halmashauri jambo ambalo litasababisha kuwa na bajeti kubwa.

“Lakini lile pendekezo la kuzisaidia Taasisi za Kiraia nalo litabebesha mzigo mkubwa wa fedha serikalini. Lakini yote yanazungumzika na yanaweza yakafanyiwa kazi,”alisema Rais Samia.

Samia alisema kupitia uchaguzi, wananchi wanapata fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka na pia uchaguzi unawafanya viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa kujiamini kwa kuwa wana ridhaa ya wananchi wanaowaongoza.

Alisema pamoja na ukweli huo, ili uchaguzi ukidhi malengo hayo, ni lazima usimamiwe vizuri na kinyume chake uchaguzi unaweza kuwa chanzo cha fujo na vurugu kama inavyotokea kwenye baadhi ya nchi.

Alipongeza NEC kwa kazi nzuri ya kusimamia na kuendesha vizuri uchaguzi wa mwaka jana.

Baadhi ya wadau wa uchaguzi akiwamo aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Cecilia Mmanga, alisema ripoti hiyo ya Tume ni nzuri na aliunga mkono kauli ya Rais Samia ya kuwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa.

“Wanawake tujitokeze kwa wingi uchaguzi ujao. Najua kuna tatizo la mfumo dume lakini pia tamaduni na mila zetu bado zinamwona mwanamke hawezi, baadhi ya vyama vya siasa bado vinakandamiza wanawake,”alisema Mmanga.

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo, aliunga mkono ushauri wa Rais Samia wa kutaka sheria ziangaliwe upya ili zisitumike kunyima watu haki ikiwemo kuenguliwa kwa kukosea kuandika jina pamoja na kuwa na watendaji wa NEC hadi ngazi ya halmashauri.

Viongozi mbalimbali walishuhudia makabidhiano ya ripoti hiyo kati ya Tume na Rais Samia. Miongoni mwao ni Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Katanga.

Chanzo: Habari leo
 
Mbwa kabisa ndio mapendekezo gani Sasa hayo? Yani badala ya kusema time iwe huru, wakurugenzi wa halmashauri wasihusike kwa namna yoyote ile kusimamia uchaguzi, walimu na watumishi wa umma wasiwe na majukumu ya uchaguzi Wala uteuzi wa mwenyekiti wa tume yenyewe asichaguliwe na Ccm wao wanaleta mapendekezo yakishamba kabisa yasikuwa na tija.
 
Tume ya Taifa ya UCHAGUZI (NEC) inapendekeza yafuatayo:-

1.Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuongeza ufanisi.

2.Tume iwe na watumishi wake mpaka ngazi ya Wilaya.

3.Kuwe na sheria moja ya Uchaguzi.

4.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume.

5.Wanaopita bila kupingwa Wabunge na Madiwani wapigiwe kura za NDIYO/ HAPANA.

6.Asasi zinazotoa elimu ya Uraia ziwezeshwe na Serikali.
Suluhisho la yote hayo ni katiba mpya
 
Mbwa kabisa ndio mapendekezo gani Sasa hayo? Yani badala ya kusema time iwe huru, wakurugenzi wa halmashauri wasihusike kwa namna yoyote ile kusimamia uchaguzi, walimu na watumishi wa umma wasiwe na majukumu ya uchaguzi Wala uteuzi wa mwenyekiti wa tume yenyewe asichaguliwe na Ccm wao wanaleta mapendekezo yakishamba kabisa yasikuwa na tija.

Wasamehe maana hawajui walitendalo.
 
Ni kama wanapendekeza iundwe Tume Huru ya uchaguzi!
Ni kama vile tume huru ipo muda mrefu ndio maana kina Mbowe, Zito, Sugu, Kubenea, Lisu, Mnyika, Msigwa, Lema na wengineo wengi kutoka upinzan waliweza kushinda chaguzi zaidi ya tatu mfululizo. Ila tatizo lililopo ni kwamba watanzania wa sasa sio wale wa 1999. Wengi wanajitambua na kuijua siasa vizuri, ndio maana hawako tayar kurubuniwa na wanasiasa uchwara anymore.

Huwezi kuja kugombea jimbo la hai afu ukishapata ushindi unakimbilia dar na dubai huku ukituacha wana hai hatuna maji, barabara, hospital wala kisima cha maji safi. Afu utegemee kila uchaguzi utakuja tukuchague. Jimbo hili haliwezi kufanywa shamba la bibi na mchumia tumbo yoyote!!!
 
Nimesoma id yako inalandana na hiki ulichokiandika hapa wewe ni dudumizi
 
Mbwa kabisa ndio mapendekezo gani Sasa hayo? Yani badala ya kusema time iwe huru, wakurugenzi wa halmashauri wasihusike kwa namna yoyote ile kusimamia uchaguzi, walimu na watumishi wa umma wasiwe na majukumu ya uchaguzi Wala uteuzi wa mwenyekiti wa tume yenyewe asichaguliwe na Ccm wao wanaleta mapendekezo yakishamba kabisa yasikuwa na tija.
Teteteteteee!
Unataka watemeshwe ugali. Na hizi tozo zinazokuja kwa kasi ya 6G nani atawalipia!

Thubuuutuu!
 
Ni kama vile tume huru ipo muda mrefu ndio maana kina Mbowe, Zito, Sugu, Kubenea, Lisu, Mnyika, Msigwa, Lema na wengineo wengi kutoka upinzan waliweza kushinda chaguzi zaidi ya tatu mfululizo. Ila tatizo lililopo ni kwamba watanzania wa sasa sio wale wa 1999. Wengi wanajitambua na kuijua siasa vizuri, ndio maana hawako tayar kurubuniwa na wanasiasa uchwara anymore.

Huwezi kuja kugombea jimbo la hai afu ukishapata ushindi unakimbilia dar na dubai huku ukituacha wana hai hatuna maji, barabara, hospital wala kisima cha maji safi. Afu utegemee kila uchaguzi utakuja tukuchague. Jimbo hili haliwezi kufanywa shamba la bibi na mchumia tumbo yoyote!!!
tukuchague. Sahau!!!
Mawazo ya Dudumizi hayana tofauti na mdudu dudumizi.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Wanatuona sisi mafala kama wao. Wao wenyewe wamesimamia wizi Oktoba 2020. Eti leo wanatoa maoni ya jinsi ya kuzuia wizi. Mafala wao wenyewe wanaondaa uchaguzi huku wakiwa na kura nyingine kwenye vikapu kwa ajili ya CCM.
Mwizi anapokupa ushauri namna ya kuzuia wizi, mwenye akili unachoweza kufanya ni kumpuuza.

Hiyo tume nzima, ni ujinga mtupu.
 
Tume ya Taifa ya UCHAGUZI (NEC) inapendekeza yafuatayo:-

1.Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuongeza ufanisi.

2.Tume iwe na watumishi wake mpaka ngazi ya Wilaya.

3.Kuwe na sheria moja ya Uchaguzi.

4.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume.

5.Wanaopita bila kupingwa Wabunge na Madiwani wapigiwe kura za NDIYO/ HAPANA.

6.Asasi zinazotoa elimu ya Uraia ziwezeshwe na Serikali.
Wanajijengea historia chafu tu hakuna kingine
 
Tume ya Taifa ya UCHAGUZI (NEC) inapendekeza yafuatayo:-

1.Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuongeza ufanisi.

2.Tume iwe na watumishi wake mpaka ngazi ya Wilaya.

3.Kuwe na sheria moja ya Uchaguzi.

4.Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume.

5.Wanaopita bila kupingwa Wabunge na Madiwani wapigiwe kura za NDIYO/ HAPANA.

6.Asasi zinazotoa elimu ya Uraia ziwezeshwe na Serikali.
Kuwe hakuna mgombania apite bila yakupingwa ila pale vyamahavikutaka kusimamisha mgombea.

Lakini ikiwa chama kimesimamisha mgombea basi ipite hekima asienguliwe na kama mgombea hakurejesha fomu au ana hitilafu fulani ya kisharia basi chama kiaarifiwe na walete mgombea mwingine badala ya kumuenguwa na kuwacha nafasi wazi ili mgombea mwingine apite bila ya kupingwa.
 
Back
Top Bottom