Tume ya Uchaguzi(NEC), yapendekeza Sheria ya Uchaguzi irekebishwe ili kuleta ufanisi

Tume ya sasa ni takataka kama takataka nyingine tu, tume inapaswa kuwa independent isiyoweza kuingiliwa na serikali.
Ungetuambia ni kwa namna gani Tume sio independent ingependeza zaidi otherwise haya mapendekezo wanayotaka Tume ndio mambo ambayo muda wote wananchi na wadau wanazitaka.
 
Huu ni mkakati wa aliejipanga kugombea 2025 anataka kuweka mizizi mpaka kwenye balozi za nyumba kumikumi,kuna watu wana mahesabu makali sana,hii mikkati ikipita jamaa anapata uraisi yaani timu yake nzima inaiteka dola.
 
Ni mapendekezo mazuri lakini tume ikiendelea kuteuliwa na mwenyekiti wa chama tawala ambaye pia ni mgombea mtarajiwa, Tume hiyo haitakuwa huru hata kama itakuwa na ofisi mpaka ngazi ya kata!
Pia suala la mgombea kupita bila kupingwa lifutwe katika mfumo huu wa vyama vingi lifutwe kabisa! Sheria itamke kuwa endapo mgombea atakosa mpinzani, mchakato husika urudiwe upya mpaka mpinzani apatikane! Na kama bado atakosekana , basi uchaguzi katika jimbo/kata husika uahirishwe kwa muda mpaka vyama vingine vitakapokuwa tayari kusimamisha wagombea!
Pia tume iweke utaratibu wa kupokea maombi ya wananchi wanaotaka kumuondoa madarakani kiongozi aliyeshindwa kutimiza majukumu yake kila ifikapo nusu ya muda wa kutawala.
 
Tume ya uchaguzi (NEC)haitakiwi kuwa na wafanyakazi wa kudumu kwa ajili ya kusimamia uchaguzi. Uchaguzi ni mchakato...is a process. NEC itawajibika kuwaajiri kwa muda (on temporary basis) wasimamizi wa uchaguzi kwa muda mwafaka. Hivyo suala la budget haliwezi kuwa shida. Nchi nyingi zinafanya hivi...wakati wa uchaguzi ukiwadia watu wenye sifa za kuwa returning officers na wote watakaosimamia uchaguzi wataomba hizi kazi kwa NEC kwa kipindi maalumu na baada ya uchaguzi kumalizika mkataba unaishia hapo. Hii ni gharama ya kawaida kama nchi inataka kutenda HAKI, kuleta maendeleo na amani kwa raia wake.
 
Sheria mpya ya Uchaguzi isisahau kupiga marufuku wakurugenzi na wateule wa mwenyekiti wa ccm kusimamia chaguzi.
Sheria hiyo pia ianzishe utaratibu kwamba mbunge/diwani akiacha kiti wazi kwa sababu zozote zile, basi mgombea aliyeshika afasi ya pili katika uchaguzi husika diye aapishwe kushika kiti hiko na kusiwepo uchaguzi wa marudio kwani unatuingiza gharama zisizo za lazima!
 
Ungetuambia ni kwa namna gani Tume sio independent ingependeza zaidi otherwise haya mapendekezo wanayotaka Tume ndio mambo ambayo muda wote wananchi na wadau wanazitaka.
Sick[emoji10], hivi hata kwa uelewa mdogo unashindwa kufahamu ya kuwa tume ikiwa huru haitawezekana kuiwekea pressure or rather watumishi kuwekewa pressure na serikali(chama kilicho madarakani) na kutokuogopa kupoteza ajira kwa kutofuata matakwa ya serikali(chama kilicho madarakani).
Tume huru inakuwa na nguvu ya kuweka fair ground bila kumuogopa yoyote, understanding this is simple and plain.
 
Mwenyekiti wa tume alipaswa kumweleza rais kuwa, unapomteua mwenyekiti na mkurugenzi wa uchaguzi - hawawi huru na hata wakiwa huru, hawawezi kuonekana wako huru. Ni vigumu, binadamu ameumbwa na aibu. Mwambie Mwenyekiti na Mkurugenzi wa uchaguzi, wachaguliwe na chombo huru kwa mfano kamati itakayojumuisha wanasheria na vyama vyote vya siasa.
Pia kamati zote za uchaguzi ngazi zote ziwe na vyama vyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…