Oktoba 21, 2025 Tume ya Uchaguzi nchini Uganda ilitangaza kuwa uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 15 Januari 2025, ikithibitisha rasmi tarehe ya wananchi kuchagua rais na wabunge wapya amabapo kwa sasa mikutano ya vyama imekuwa ikiendelea
Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81 na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, alitangaza azma yake ya kugombea tena urais. Museveni, ambaye ni miongoni mwa viongozi waliodumu muda mrefu zaidi madarakani barani Afrika, amewahi kubadilisha katiba mara mbili – kuondoa ukomo wa mihula na kikomo cha umri wa kugombea urais
Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa nyota wa muziki aliyegeukia siasa, Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi. Bobi Wine amekuwa akitumia umaarufu wake katika muziki kuwavuta vijana wengi wanaotaka mabadiliko
Katika uchaguzi wa mwaka 2021, Bobi Wine aligombea dhidi ya Museveni na kudai kuwa matokeo yalighushiwa kupitia kujaza kura, vitisho kwa wapiga kura, rushwa, na udanganyifu mwingine wa uchaguzi. Hata hivyo, chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kilikanusha tuhuma hizo
Zaidi ya wagombea wengine sita kutoka vyama vidogo nao wamejitokeza kuwania urais, huku Wananchi pia wakitarajiwa kuwachagua wabunge wapya katika uchaguzi huo mkuu
Source: African news & Spout TV