Pre GE2025 Tume ya Uchaguzi: Wapigakura milioni 34.7 wanatarajiwa kushiriki Uchaguzi mkuu Oktoba

Pre GE2025 Tume ya Uchaguzi: Wapigakura milioni 34.7 wanatarajiwa kushiriki Uchaguzi mkuu Oktoba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akizungumza leo Machi 5, jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Kailima Ramadhani Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema kuwa jumla ya wapigakura 34,746,638 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume, idadi hiyo inatokana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura unaoendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini.

View attachment 3259708
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani
Soma, Pia
Huyu si yule tangu zama za JK? Wezi wale wale
 
Kwenye zoezi la uboreshaji na kupata kitambulisho la siku 7 linaloendelea hapa Morogoro Manispaa litawaacha watu wengi bila ya kupata huduma hatimaye kushindwa kipiga kura mwezi October. Watu ni wengi wanaohitaji vitambulisho na vituo vingi vina machine( BVR) moja ambazo hazina speed na mara kwa mara zinasimama. Wananchi wengi hawana vitambulisho vya NIDA kwa kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa kwaiyo wanavitumia vitambulisho vya kupigia kura kama mbadala. Tume Uchaguzi iongeze muda kutoka siku 7 hadi siku 14
 
Tume ya Uchaguzi: Mkoa wa Kilimanjaro, haikusajili zaidi ya watu 30,000 kisa, muda ulikuwa mfupi,Leo wanakuja na idadi kubwa kumbe haikuandikisha watu wote
 
Waliopo eligible ni wangapi ?

Siasa duniani pote kwa sasa watu wengi hawashiriki, kwahio haijawahi kutokea 100 percent wote wakashiriki.., na hata kupata 50 percent huwa ni shida kwa kwa mambo yalivyo sasa sidhani hata 30 watashiriki watu wameshachoka na huu usanii kwahio they don't care na watu huwa wanajiandisha ili kupata kitambulisho na sio kingine...
 
Tanzania: Age structure from 2013 to 2023
Characteristic0-14 years15-64 years
202342.72%54.23%
202242.92%54.05%
202143.13%53.84%
202043.37%53.61
 
Ina maana kuwa watanzania wote kuanzia umri wa miaka 18 nchini Tanzania wamejiandikisha.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa za kigogo Kailima Ramadhani wa INEC - "Kwa mujibu wa taarifa ya Tume, idadi hiyo inatokana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura unaoendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini" mwisho wa kumnukuu.

1741340455281.jpeg


View: https://m.youtube.com/watch?v=Ud9RzltN-jA
 
Back
Top Bottom