Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Ni kweli kuwa hatukuwahi kuwa na sakata la kuengua enguana kwenye chaguzi chaguzi hizi tokea tupate uhuru. Pia, ni kweli kuwa engua enguaji ya kwanza ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza kwenye chaguzi za tawala za serikali za mitaa zinazoendeshwa chini ya tamisemi. Hizi ilikuwa ni katika chaguzi hizo ndani ya awamu ya 5.
Kwenye hali ya kufanana kama iliyopo sasa, wagombea uchaguzi wa upinzani kwa mamia na maelfu walienguliwa hali hakukuwa na mgombea hata mmoja aliyeenguliwa kutoka chama tawala yaani chama baba lao.
Kimsingi ilikuwa mithili ya kuilazimisha timu moja kuweka mpira kwapani kabla ya muda kwisha. Ndicho kilichotokea, hatimaye upinzani kuamua kuweka mpira kwapani!
Kwa hakika uchaguzi ule uliipaka sana nchi yetu hii pendwa matope machoni mwa jumuiya ya kimataifa. Katika angalau kuokoa jahazi, waziri wetu makini, mtalaamu wetu mahiri wa kupiga nyungu, alitangaza kuondolewa kwa pingamizi zote na bila masharti yoyote ili kuwarejesha wagombea wote kwenye sanduku. Hii ikiwa ni kwa ajili ya kulinda mustakabala mwema wa nchi yetu.
Kongole kwako Selemani Jaffo japo hatua yako ilikuja kwa kuchelewa mno.
Halipo somo kwa tume ya uchaguzi kuhusiana na hili ikizingatiwa kuwa labda yawezekana hatutaki kuona kuwa tupo njia panda?
Kwa nini kujiweka katika hatari tusiyoijua au kujitumbukiza bure kwenye tafrani ambayo mwenye kutaka kutwambia hatima yake kwa hakika atakuwa ni mwongo wa wazi?
Walisema waungwana "usipoziba ufa, utajenga ukuta."
Chonde chonde tungali nayo nafasi ya kurekebisha mambo vilivyo kabla ya kuchelewa mno.
Nafasi ya kuuziba ufa ingalipo japo haitadumu sana.
Waungwana wanasisitiza: "chelewa chelewa utakuta mwana si wako."
Ninawasilisha.