Tume ya uchaguzi yasitisha kutangaza matokeo kupisha uchunguzi wa fomu za 34A

Tume ya uchaguzi yasitisha kutangaza matokeo kupisha uchunguzi wa fomu za 34A

Wakipindua matokeo yaliyokwisha tangazwa itakuwa balaa zaidi...
Hilo balaa halitoiacha Kny salama...
Hata hali hii tu yenyewe haitaiacha nchi salama. Haina tofauti na maamuzi ya TEF ya jana kwa wahariri wa vyombo vya habari vya watanzania
Nilishangazwa na tume kutangaza priminary results haraka haraka wakati wakijua fika kwamba wamekihuka kanuni za chaguzi, kulikuwa na ulazima gani wa kuharakisha mambo?

Kuuwawa kwa Mkurugenzi mkuu wa ICT wa tume ya uchaguzi na kukutwa mwili wake umekatwa mkono, si hilo tu hata wataalamu/washauri wa ICT kutoka Marekani na Canada walitiwa mbaroni nafikiri wamekwisha wa deport - kwa akili za kawaida matukio hayo yote yalikuwa na lengo gani kama si ushahidi tosha kwamba Dola lilikuwa lina mpango wa kuingilia system ya upigaji kura na ku-favour Kenyatta? Siwatakii mabaya Wakenya lakini Serikali yao isitake kulazimisha mambo ambayo yanaweza kuikosesha amani Kenya na raia wake - hakuna haja ya kulazimisha ushindi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom