PostGE2025 Tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 yakutana na vyama vya siasa nchini

PostGE2025 Tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 yakutana na vyama vya siasa nchini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
​
TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 22, 2026, imekutana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
-
Mkutano huo wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa nchini umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.
-
Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
-
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa matukio hayo.

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

1769081039126.png

1769081214914.png

​
 
Ukumbi wanaotumia ni pale BOT Unategemea nini?
hawa pimbi mpaka miaka mitano iishe wanakula kiyoyozi na posho nene tu mapimbi haya!

Hata mm ningekua mwenyekiti wa Tume ninge prolong hilo zoezi mpaka mwakani.

Nikimaliza hapa ndani naenda kuhoji na Nchi jirani, si mlisema vijana walitoka nje?
Napita kenya, Uganda & Rwanda.

Then naapita kwa nchi za Mabalozi woote walio kua wana issue waraka wa kabla na baada ya matukio.

Alafu namalizia Vyombo vya habari.

Yote hii ningefanya ili Nifaidi Perdiemu Nzuri, Maana hata ukiwa serious na kazi vipi No. body will give the fvck about your report or recommendations
 
Unadhani ana uhuru huo basi. Hata kesho akiambiwa afunge ofisi akabidhi ripoti hana cha kubisha. Wao lao moja, kubangaiza huku na huko ili kuwachelewesha ICC.
 
Utadhani wapo serious na maisha kumbe hapo wanajiona kama Kanumba kipindi cha kaole akiigiza kuwa kwenye tume.

Upuuzi mtupu.
Wamekuwa waigizaji wazuri. Sijui walipitia pale TASUBA wakanolewa kidogo au wana vipaji vya asili?
 
Wanatupotezea muda tu,maelekezo wanayo kupitia hadidu za rejea zs samuya.
 
Hata mm ningekua mwenyekiti wa Tume ninge prolong hilo zoezi mpaka mwakani.

Nikimaliza hapa ndani naenda kuhoji na Nchi jirani, si mlisema vijana walitoka nje?
Napita kenya, Uganda & Rwanda.

Then naapita kwa nchi za Mabalozi woote walio kua wana issue waraka wa kabla na baada ya matukio.

Alafu namalizia Vyombo vya habari.

Yote hii ningefanya ili Nifaidi Perdiemu Nzuri, Maana hata ukiwa serious na kazi vipi No. body will give the fvck about your report or recommendations
Umesahau na safari ya kwenda Vatican maana hadi Papa aliguswa na yanayoendelea bongo.
 
Back
Top Bottom