BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, mjadala kuhusu mwenendo na matukio yaliyohusisha uvunjifu wa haki za binadamu umeendelea kushika kasi ndani na nje ya Tanzania.
Malalamiko kutoka kwa wadau wa ndani, asasi za kiraia, pamoja na Jumuiya za Kimataifa yaliibua hitaji la uchunguzi huru na wa kina.
Katika mazingira hayo, Rais Samia alitangaza kuundwa kwa Tume maalumu ya kuchunguza matukio hayo, hatua ambayo kwa upande mmoja ilionekana kuwa ya kujenga, lakini kwa upande mwingine ilizua maswali makubwa kuhusu uhalali, uwazi na uhuru wa Tume hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Changamoto na mashaka yanayoelekezwa kwa Tume hii yanatokana na sababu kadhaa za msingi ambazo zimekuwa zikijirudia katika historia ya taasisi kama hizi nchini.
1. Muundo wa Tume Ulivyo: Je, Unawakilisha Wadau Wote?
Msingi wa kwanza wa ukosoaji unatokana na muundo wa Tume yenyewe. Wadau wengi wanaamini kuwa kuweka wazee wastaafu wa serikali ambao utumishi wao wa mwisho ulikuwa ndani ya mifumo ambayo inadaiwa kuhusika katika malalamiko hayo, hali hiyo inadaiwa kuwa kunapunguza hadhi ya Tume kama chombo huru.
Hoja hii ina mizizi katika dhana ya mgongano wa maslahi, ambapo wananchi wanahoji: inawezekana vipi watu waliokulia katika mfumo huo huo wawe sehemu ya uchunguzi wa mfumo huo? Kutokuwepo kwa wawakilishi wa asasi za kiraia, wanataaluma huru, makundi ya kijamii na wachambuzi binafsi kunachukuliwa kama pengo linaloathiri usawa na uaminifu wa Tume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka akizungumza Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, tarehe 20 Novemba, 2025
2. Uhuru wa Tume na Hofu ya Mwingiliano wa Kisiasa
Chanzo kingine cha kutokuaminika ni wasiwasi kuhusu uhuru wa Tume. Tanzania imekuwa na historia ya taasisi huru zinazolalamikiwa kuathiriwa na mamlaka ya juu kisiasa, hasa pale wajumbe wanapopatikana kwa teuzi za moja kwa moja za Rais.
Hali hii imewafanya baadhi ya wadau kuona kuwa ni rahisi kwa Tume “kuwekewa matokeo,” jambo linalopelekea sintofahamu kuhusu uwezo wake wa kutoa matokeo yasiyopendelewa na mhimili wa utawala.
3. Je, Tume ina uwezo wa kubisha hodi kwa kila anayeshtumiwa?
Wasiwasi mwingine ni uwezo wa Tume kufikia mamlaka na taasisi zote zinazohusika kwa namna moja au nyingine na matukio yanayodaiwa kutokea. Kwa kuwa baadhi ya tuhuma zinagusa vyombo vya dola na viongozi wenye nguvu, wadau wanahoji kama Tume inaweza kuwafikia bila shinikizo au kuwekewa mipaka.
Hofu ya baadhi ya wadau ni kuwa maeneo yenye ushahidi muhimu yanaweza kubaki nje ya uchunguzi kutokana na vikwazo vya kimamlaka.
4. Historia ya Tume Nchini: Je, Inaacha Somo Gani?
Historia imekumba Tume nyingi zilizoundwa kuchunguza matukio nyeti nchini; mara nyingi ripoti zao zimenyoshewa kidole kuwa zina “matobo” au zimewekwa katika makabati bila utekelezaji. Kutokana na rekodi hii, wananchi wanaona Tume ya sasa kama mwendelezo wa mfumo ule ule wa kutumia Tume kama “kifaa cha kupooza mjadala” bila kusababisha mabadiliko ya kweli ambayo yamekuwa yakilalamikiwa.
5. Uwajibikaji wa Ripoti: Nini kitatokea baada ya ripoti?
Hata kama Tume itafanya kazi kwa nidhamu, bado swali kubwa linabaki: ripoti yake itasababisha nini? Wadau wengi wanaamini kuwa ripoti za Tume mara nyingi hukosa meno ya uwajibikaji na kwamba matokeo yake hayatengenezwi kwa lengo la kubadili mifumo bali kufunika shinikizo la kisiasa.
6. Tume Kwa Mkakati au Shinikizo Kimataifa:upi misingi wa kuundwa kwake?
Uwepo wa wataalamu wa usalama, sheria na diplomasia umewafanya wengine kuona Tume hiyo kama chombo cha kimkakati cha kupunguza presha kutoka jumuiya za kimataifa. Kwa mtazamo huu, wengine wanaona Tume imeundwa ili kutoa taswira ya uwajibikaji wa kiserikali kuliko kushughulikia chanzo halisi cha matatizo.
Wapo wadau katika mijadala wanasema kwamba ili kujenga imani, Tume ya uchunguzi hasa kwa masuala nyeti kama haki za binadamu, lazima iwe na muundo shirikishi, uongozi huru, uwezo wa kufika kila mahali, na dhamira ya kweli ya kufikisha ukweli kwa umma. Bila hivyo, Tume yoyote itaonekana kama kiini macho kuliko chombo cha haki.
Kwa muktadha huo, nini kinaweza kutarajiwa?
Katika mazingira haya, swali linalosalia mezani ni iwapo Tume hiyo itaweza kuvuka vikwazo vilivyo mbele yake na kuanzisha mwelekeo mpya wa matumaini kwa Tume za ndani, au kama itaendelea kuamsha hisia na madai ya haja ya Tume Huru kutoka nje ya nchi katika kushughulikia masuala nyeti.
Huenda hili ndilo jaribio kuu au mtego kwa Serikali na watawala, katika safari ya kujenga upya msingi wa kuaminika na kuaminiana. Ni mtihani utakaobainisha iwapo taasisi zetu zina uwezo wa kuanzisha imani mpya kwa umma, au kama zitaendelea kukabili shaka iliyojengeka kuhusu uwajibikaji na uthabiti wa maamuzi katika masuala ya msingi.