KERO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Jana mheshimiwa Rais Samia amezindua rasmi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo Ina majukumu ya Kulinda na kutunza faragha za watu.

Sasa Kuna mtindo umezuka ambapo Online Creditors Wamekuwa wanasambaza taarifa binafsi za Wateja Wao Kwa watu mbalimbali ambao Huwa wanawasiliana Kwa kuwapigia na kutoa kashfa na kueleza kwamba wanamdai mhusika.Watu wengi wamekuwa wanalalamika Kwa huu upuuzi unaofanywa na Hawa wakopeshaji wa kimtandao.

Hii tabia sio tuu inakiuka faragha Bali inakiuka Haki ya mteja. Kama walikibaliana kulipana na mteja hajatimiza matakwa Kwa nini hawafuati masharti yaliyopo kwenye makubaliano Yao? Hii tabia ya kuidhalilisha wateja imetoka wapi?

Nitoe wito Kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ichukue hatia Kali Kwa TCRA,Benki Kuu na Mitandao ya Simu Kwa kuyotimiza wajibu wao badala yake wanakiuka Haki za mteja.

---

Wakopaji mtandaoni wanavyodhalilishwa​

“Dawa ya deni kulipa,” ni msemo unaotumiwa na watu wengi wanaodai fedha zao wakimaanisha ili kumalizana ni lazima mdaiwa alipe kile alichokopeshwa.

Mbali na msemo huo, hivi sasa watu hukumbushwa kulipa deni kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) kwenye simu ya mhusika na kupitia watu wengine, ambao mkopaji anawasiliana nao mara kwa mara, haijalishi ndugu wala rafiki zake.

Kutokana na watu wengi kuwa uhitaji fedha, kumekuwepo na aplikesheni nyingi mtandaoni za mikopo ya ‘chapchap’ na kila moja ikiwa na kiwango chake, lakini zote zikinadi ni mkopo nafuu na wa haraka bila masharti.

Chanzo: Mwananchi

My Take: Ni vile watu hawajui sheria na pa kuanzia ila jambo hili likigikishwa mahakamani ni wazi wahusika watalipishwa faini na fidia Kwa damage wanayofanyia wateja.

Pia soma malalamiko mengine: KERO - Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Majibu ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yazionya Taasisi za mikopo zinazodhalilisha watu ikiwemo kutuma ujumbe kwa ndugu
 
Ukikopa lipa deni kadri ya makubaliano. Mnakopa halafu hamrudishi deni, mkipigiwa simu hamupokei. Unadhani hayo makampuni hayapati hasara?

Halafu pili kuna terms and conditions kila unapoingia kwenye mikopo ya Online. Wengi hawasomi hicho kipengele. Sheria hii ya PIPA haitakusaidia kitu as long as umekubali impliedly kuwa kama hautalipa watawa contact watu wako wa karibu
 
Akili za kijinga kama hizi ndio zitawaponza.

Biashara ya kukopesha na kudai Kuna taratibu zake.
 
Mjinga hajijui kuwa mjinga ila watu wengine wote wanamuona kuwa ni mjinga.

Yaani wewe kapuku ambaye huna fedha unajifanya unajuwa sheria kuliko wale wlio licensed na BOT?? Au kwa kuwa una uwezo wa kununua bando ndiyo wajifanya mjuwaji.

Lipa madeni au acha kukopa ndiyo dawa otherwise tutaendelea kukuumbua tu kama ChoiceVariable au fallacy
 
Ukikopa lipa deni kadri ya makubaliano. Mnakopa halafu hamrudishi deni, mkipigiwa simu hamupokei. Unadhani hayo makampuni hayapati hasara?

Halafu pili kuna terms and conditions kila unapoingia kwenye mikopo ya Online. Wengi hawasomi hicho kipengele. Sheria hii ya PIPA haitakusaidia kitu as long as umekubali impliedly kuwa kama hautalipa watawa contact watu wako wa karibu
Ww ndio mwenye hizo kampuni uchwara
 
Mi wanachoniudhi suala la kudukua taarifa zako binafsi ikiwemo picha na video, hii ina mahusiano gani na deni unalonidai?

Halafu wanatishia kusambaza na sometime kuziuza nje ya nchi. huu ni zaidi ya udhallishaji.

Kama hujalipwa nenda polisi sio kudhalilisha watu.
 
"Kukopa fedha na kutotaka kurejesha ili wengine wanufaike ni kitendo cha fedhea, kudaiwa siyo fedhea labda fedhea ujitakie mwenyewe "
sisi hatukatai kudaiwa, tunachosema kwa nini utoe faragha za watu, mlikubaliana hilo suala wakati unamkopesha mteja wako?
 
mi wanachoniudhi suala la kudukua taarifa zako binafsi ikiwemo picha na video, hii ina mahusiano gani na deni unalonidai?

halafu wanatishia kusambaza na sometime kuziuza nje ya nchi. huu ni zaidi ya udhallishaji.

kama hujalipwa nenda polisi sio kudhalilisha watu.
Hizo picha wanadukya au unawaoa wewe unapoomba Mikopo , all in all , ni wapuuzi sana!
 
Kukopa Ni Siri ya mkopaji na mtoa mkopo.
Aidha mkopeshaji aunde kundi lake la wakopeshwaji halafu akalisajili.
 
Mimi binafsi baada ya kupokea simu yenye kejeli, vitisho na dharau kutoka kwa wakopeshaji niliamua kutowalipa laki nabushee. Nawasibiri waniburuze mahakamani Ila wajue msg zao za matusi bado ninazo
 
na wengi wao wanaojihusisha na hizi kampuni za kutoa mikopo midogo ni wanawake wapo wengi sana
 
Mimi binafsi baada ya kupokea simu yenye kejeli, vitisho na dharau kutoka kwa wakopeshaji niliamua kutowalipa laki nabushee. Nawasibiri waniburuze mahakamani Ila wajue msg zao za matusi bado ninazo
Ni vile ni wajinga,hawajui kwamba wanafanya vitendo vya kuvunja sheria na wakifunguliwa kesi wanaweza lipa fidia na vikampuni vyao vikafungwa.

Wafuate taratibu za kisheria za kudai sio ujinga wanaoufanya
 
"Mfumo wa faragha naishauri serekali iuondoe kwenye baadhi ya taasisi kama mabenki, na taasisi za kifedha, zitakufa.
Kwani wanachokifanya hao Wakopeshaji unaona ni sahihi? Huko Ulaya watu wanaficha pesa Kwa sababu Kuna faragha
 
"Kukopa fedha na kutotaka kurejesha ili wengine wanufaike ni kitendo cha fedhea, kudaiwa siyo fedhea, ni haki ya mkopeshaji, tukope na kulipa kwa wakati, kuepuka kufedheheshwa"
Utaratibu wa kudai inakiuka Haki ya faragha za watu na hauko Kwa mujibu wa sheria ndicho watu wanakilalanikia sio kutolipa.

Kuna njia za kumuwajibisha asiyelipa.
 
Jana mheshimiwa Rais Samia amezindua rasmi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo Ina majukumu ya Kulinda na kutunza faragha za watu.

Sasa Kuna mtindo umezuka ambapo Online Creditors Wamekuwa wanasambaza taarifa binafsi za Wateja Wao Kwa watu mbalimbali ambao Huwa wanawasiliana Kwa kuwapigia na kutoa kashfa na kueleza kwamba wanamdai mhusika.Watu wengi wamekuwa wanalalamika Kwa huu upuuzi unaofanywa na Hawa wakopeshaji wa kimtandao.

Hii tabia sio tuu inakiuka faragha Bali inakiuka Haki ya mteja. Kama walikibaliana kulipana na mteja hajatimiza matakwa Kwa nini hawafuati masharti yaliyopo kwenye makubaliano Yao? Hii tabia ya kuidhalilisha wateja imetoka wapi?

Nitoe wito Kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ichukue hatia Kali Kwa TCRA,Benki Kuu na Mitandao ya Simu Kwa kuyotimiza wajibu wao badala yake wanakiuka Haki za mteja.

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1774848738290188590?t=7TkELfmQcCU4e96SX2mWIQ&s=19

My Take: Ni vile watu hawajui sheria na pa kuanzia ila jambo hili likigikishwa mahakamani ni wazi wahusika watalipishwa faini na fidia Kwa damage wanayofanyia wateja.

View: https://www.instagram.com/p/C5TEsort5sR/?igsh=MWx2N3p1a2hqa3Q4bw==

Dawa ya deni ni kulipa tu.
 
Back
Top Bottom