KERO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika

KERO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jana mheshimiwa Rais Samia amezindua rasmi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo Ina majukumu ya Kulinda na kutunza faragha za watu.

Sasa Kuna mtindo umezuka ambapo Online Creditors Wamekuwa wanasambaza taarifa binafsi za Wateja Wao Kwa watu mbalimbali ambao Huwa wanawasiliana Kwa kuwapigia na kutoa kashfa na kueleza kwamba wanamdai mhusika.Watu wengi wamekuwa wanalalamika Kwa huu upuuzi unaofanywa na Hawa wakopeshaji wa kimtandao.

Hii tabia sio tuu inakiuka faragha Bali inakiuka Haki ya mteja. Kama walikibaliana kulipana na mteja hajatimiza matakwa Kwa nini hawafuati masharti yaliyopo kwenye makubaliano Yao? Hii tabia ya kuidhalilisha wateja imetoka wapi?

Nitoe wito Kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ichukue hatia Kali Kwa TCRA,Benki Kuu na Mitandao ya Simu Kwa kuyotimiza wajibu wao badala yake wanakiuka Haki za mteja.

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1774848738290188590?t=7TkELfmQcCU4e96SX2mWIQ&s=19

My Take: Ni vile watu hawajui sheria na pa kuanzia ila jambo hili likigikishwa mahakamani ni wazi wahusika watalipishwa faini na fidia Kwa damage wanayofanyia wateja.

View: https://www.instagram.com/p/C5TEsort5sR/?igsh=MWx2N3p1a2hqa3Q4bw==

Ina maana wale wadukuaji wa mawasiliano ya watu wamepata muarobaini.
 
We lipa deni mkuu. Ukilipa wàtu wako wa karibu hawatapewa taarifa zako kwamba unadaiwa.
Mnawakuta wajinga,hizi stori niliziona kwenye gazeti hapo na mtu akanisimulia mtaani.

Mimi ukifanya hivyo ujiandae Kupeleka wakili mahakamani
 
Mnawakuta wajinga,hizi stori niliziona kwenye gazeti hapo na mtu akanisimulia mtaani.

Mimi ukifanya hivyo ujiandae Kupeleka wakili mahakamani
Ushindwe kulipa deni halafu upate hela ya kulipa wakili??
 
Nafanya hii biashara ya kukopesha nimejifunza vingi sana kwanza hakuna watu wasioogopa madeni kama Wanaume😃hawaogopi kudaiwa.

Sijajua huyo alieleta hii system ya kutumia watu meseji alifikiria haijakaa sawa hata kidogo, wabongo ni wa kudeal nao kimtaa!

Sikupeleki polisi wala mahakamani ila pesa yangu utalipa tu!!!
 
Sawa, kwa uzoefu wako hao jamaa wanaofedhehesha watu kwa kutuma sms je, baada ya hapo wanampeleka wapi mdaiwa?
 
Nadhani ukitaka kuwashitaki vizuri uwalipe deni lao kwanza,then nawewe uanze kuwadai fidia ya udhalilishaji walioufanya. Maana kuchelewa kulipa deni ni kawaida. BTW,ni baada ya muda gani kupita bila kulipa ndio wanaanza kuwatumia watu SMS?
 
That was exactly my thoughts too nilipoona wanaizindua, kuna mikopo imekuwa zaidi ya dhoruba kwa wakopaji.
 
Nadhani ukitaka kuwashitaki vizuri uwalipe deni lao kwanza,then nawewe uanze kuwadai fidia ya udhalilishaji walioufanya. Maana kuchelewa kulipa deni ni kawaida. BTW,ni baada ya muda gani kupita bila kulipa ndio wanaanza kuwatumia watu SMS?
Mtoa mada anamaana kwanza taarifa za mkopaji zilindwe ili zisitumiwe vibaya na hao wakopeshaji kudhalilisha watu meaning data privacy wanazokusanya kwa app zao zianze kuwa restricted kutumika bila kufata sheria za taarifa binafsi
 
dawa ya deni ni kulipa
Leo unaona wako sawa kwa sababu wanadhalilisha ambao hawajalipa ila kesho wakianza ku blackmail watumiaji wote wa hizo app kwa taarifa walizokusanya sijui kama utasema kama wako sahihi. Data privacy na data protection centres lazima zitungiwe sheria kali sana.
 
Mtoa mada anamaana kwanza taarifa za mkopaji zilindwe ili zisitumiwe vibaya na hao wakopeshaji kudhalilisha watu meaning data privacy wanazokusanya kwa app zao zianze kuwa restricted kutumika bila kufata sheria za taarifa binafsi
Ndio maana yake, ukute hata hizi connection zote zinatolewa na hizi app, then wanamuuzia msambaza connection.
 
We lipa deni mkuu. Ukilipa wàtu wako wa karibu hawatapewa taarifa zako kwamba unadaiwa.
Leo wanafanyia walioshindwa kulipa huo udhalilishaji na wanachekewa na kesho kama hawatadhibitiwa kwa data privacy laws watakuja blackmail hata watumiaji wote ambao wana data zao, kuweni makini na mnavyovitetea. Bodi ya mikopo haishindwi kudhalilisha inaowadai ila inajaribu kufata sheria za nchi.
 
Ndio maana yake, ukute hata hizi connection zote zinatolewa na hizi app, then wanamuuzia msambaza connection.
Exactly, madhara ya kutokemea hii michezo ya udhalilishaji ni makubwa sana huko mbele.
 
Ushindwe kulipa deni halafu upate hela ya kulipa wakili??
Inawezekana hii loophole ya kujua kwamba hamchukuliwi hatua ipo na ndo maana mnapita nayo ila trust me, hawa watu wasipodhibitiwa kesho wataanza ku blackmail watu na data za watu kama wamefikia hatua ya kufanya wanayofanya which is hawafati sheria basi watafanya mambo ya ajabu sana badae. Kuweni makini na mnavyovitetea.
 
Back
Top Bottom