Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC): Wanaosambaza taarifa binafsi za watu bila ridhaa yao kuchukuliwa hatua za kisheria

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC): Wanaosambaza taarifa binafsi za watu bila ridhaa yao kuchukuliwa hatua za kisheria

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imesema kuwa mtu au taasisi yoyote itakayobainika kukiuka faragha au kutumia taarifa binafsi bila ridhaa ya muhusika au kinyume na taratibu zilizowekwa kisheria, itawajibishwa ipasavyo bila kujali hadhi au ukubwa wake.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Mkilia, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezwa kwa muda wa nyongeza kwa taasisi zote za umma na binafsi zinazokusanya au kuchakata taarifa binafsi ambazo bado hazijakamilisha usajili wake na PDPC.

Dkt. Emmanuel Mkilia aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, Januari 22, 2026 jijini Dar es Salaam.

 
Back
Top Bottom