Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) yakanusha taarifa usajili wa CCTV kwa watu binafsi

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) yakanusha taarifa usajili wa CCTV kwa watu binafsi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imebaini kuwepo kwa taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa mitandaoni kuwa kila mwenye kamera za usalama (CCTV) anatakiwa kujisajili na Tume hiyo.

1774427960900.png
Kupitia ufafanuzi wake, Tume imeeleza kuwa si kweli kwamba kila mtu binafsi mwenye kamera za CCTV anatakiwa kujisajili.

Kwa mujibu wa sheria, wajibu wa kujisajili unawahusu taasisi zote za umma na binafsi zinazokusanya au kuchakata taarifa binafsi, ikiwemo kupitia matumizi ya CCTV, na siyo kila mtu mmoja mmoja. Taasisi hizo zinapaswa kujisajili na Tume kabla au ifikapo Aprili 8, 2026.

Soma: Serikali yapiga marufuku kutumia CCTV Camera bila usajili. Je, ni kuwalinda wasiojulikana?

Kwa upande wa matumizi ya CCTV katika makazi binafsi, Tume imeelekeza kuwa kamera zinapaswa kuelekezwa ndani ya mipaka ya eneo la mhusika pekee. Imeonya kuwa iwapo kamera zitarekodi maeneo ya nje ya mipaka hiyo, hususan maeneo ya umma, matumizi hayo yatakuwa kinyume cha sheria na mhusika atawajibika kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Tume imesisitiza umuhimu wa kuweka alama maalum (signage) zinazoonesha kuwa eneo husika lipo chini ya uangalizi wa CCTV inayokusanya taarifa binafsi, ili kulinda faragha za watu.

PDPC imeeleza kuwa itaendelea kutoa miongozo zaidi ili kuhakikisha matumizi sahihi ya teknolojia ya CCTV yanafuata sheria na kulinda haki za faragha za wananchi.
 
Sasa hivi hata ukienda kwa mtu kumsalimia Tajiri ukilala kwake usipige punyeto wanakuchora
 
Back
Top Bottom