Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Katika mambo yanayoshangaza sana nchini ni ubutu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara nchini (Fair Competition Commission, FCC). Kuna mambo mengi sana nchini yanafanywa na wafanyabiashara kwa kukiuka taratibu za 'fair competition" lakini hata siku moja hutasikia FCC wamechukua hatua.
Labda niwape mfano rahisi sana kuelewa. Umewahi kutembelea sehemu ya kupata chakula au vinywaji na ukaambiwa hapa hatuuzi CocaCola kwa sababu tuna mkataba na Pepsi, au hapa hatuuzi Pepsi kwa sababu tuna mkataba na Coca Cola? Basi huo ni ujinga mmojawapo ambao FCC hawapaswi kabisa kuuruhusu, lakini wamekaa tu kimya.
Hata suala la kupiga marufuku daladala katika njia (route) fulani, hatujasikia FCC wakitoa tamko. Bei za mafuta ya magari kufanana vituo vyote Dar es Salaam, kama FCC wangejua kazi yao wangeingilia kati - kwanini bei ziko sawa wakati bei elekezi za EWURA ziko katika range?
Kuna mambo kama bima za magari, kwanini makampuni na agents wote wa bima wana-charge kiwango elekezi cha juu cha bima za magari? FCC huwa wanajiuliza haya maswali? Wamewahi kusikia maneno "price cartels" na "price syndicates" katika kazi zao, au hicho ni kiingereza kigumu sana kwao?
Mfano mwingine ni vitu feki Tanzania. Vimejaa kuanzia madawa ya binadamu, simu, TV, computer, spare za magari, vipodozi, na kila kitu, achana na nguo nk. Na vinauzwa waziwazi utafikiri hawa wanaouza wamepewa kibali na FCC.
Hivi unajua mojawapo ya kazi za FCC ni kuhakikisha vitu feki haviingizwi nchini. Hebu niambieni jamani, nani ameshawahi kuona jitihada za FCC kupambana na vitu feki nchini?
Hii nchi ina mambo ya hovyo sana