HOJA Tume ya Ushindani wa Kibiashara nchini (FCC) inajua kweli kazi yake? Ipo kimya kwenye mambo mengi sana

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Katika mambo yanayoshangaza sana nchini ni ubutu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara nchini (Fair Competition Commission, FCC). Kuna mambo mengi sana nchini yanafanywa na wafanyabiashara kwa kukiuka taratibu za 'fair competition" lakini hata siku moja hutasikia FCC wamechukua hatua.

Labda niwape mfano rahisi sana kuelewa. Umewahi kutembelea sehemu ya kupata chakula au vinywaji na ukaambiwa hapa hatuuzi CocaCola kwa sababu tuna mkataba na Pepsi, au hapa hatuuzi Pepsi kwa sababu tuna mkataba na Coca Cola? Basi huo ni ujinga mmojawapo ambao FCC hawapaswi kabisa kuuruhusu, lakini wamekaa tu kimya.

Hata suala la kupiga marufuku daladala katika njia (route) fulani, hatujasikia FCC wakitoa tamko. Bei za mafuta ya magari kufanana vituo vyote Dar es Salaam, kama FCC wangejua kazi yao wangeingilia kati - kwanini bei ziko sawa wakati bei elekezi za EWURA ziko katika range?

Kuna mambo kama bima za magari, kwanini makampuni na agents wote wa bima wana-charge kiwango elekezi cha juu cha bima za magari? FCC huwa wanajiuliza haya maswali? Wamewahi kusikia maneno "price cartels" na "price syndicates" katika kazi zao, au hicho ni kiingereza kigumu sana kwao?

Mfano mwingine ni vitu feki Tanzania. Vimejaa kuanzia madawa ya binadamu, simu, TV, computer, spare za magari, vipodozi, na kila kitu, achana na nguo nk. Na vinauzwa waziwazi utafikiri hawa wanaouza wamepewa kibali na FCC.

Hivi unajua mojawapo ya kazi za FCC ni kuhakikisha vitu feki haviingizwi nchini. Hebu niambieni jamani, nani ameshawahi kuona jitihada za FCC kupambana na vitu feki nchini?

Hii nchi ina mambo ya hovyo sana
 
Watu wanavaa masuti na kupiga picha za kishobo lakini hatuoni kazi wanazofanya. Hebu watu wa Anti-counterfeits watuambie, kuna haja gani ya kuwa na taasisi hiyo kama Tanzania vitu feki vimejaa kila mahali? Huenda hata wao wanatumia vitu feki!
 
Kuna hapa watu wanafanya kazi kwenye Restrictive Trade Practices, wakati naenda zangu kula kitimoto na Pepsi, naambiwa hapa haturuhusiwi na Coca Cola kuuza Pepsi kwa sababu Coca Cola wamtupa viti vyao vya kukalia. Kwamba hawa hajui haya? Ovyo kabisa.
 
Wanafanya kaxi ila tatizo nchi hii inaongozwa kwa maagizo toka juu.
Mkuu sasa hicho kitakuwa kisingizio tu. Hivi maudhi ya kuambiwa hapa hatuuzi Pepsi kwa sababu tumepewa viti na Coca Cola ni jambo la maagizo toka juu?

Maagizo toka juu tunaweza kuyaelewa katika suala la daladala kupigwa marufuku ili kampuni ya mwendokasi ya mjomba ipate wateja. Lakini baa za Temeke?
 
Mkuu hayo mengine sijui ila mafuta nakukatalia.

Bei ya mafuta inapangwa ukomo yaani usiuze bei juu ya iliotajwa. Vipo vituo vinauza chini ya bei elekezi.
 
Mkuu hayo mengine sijui ila mafuta nakukatalia. Bei ya mafuta inapangwa ukomo yaani usiuze bei juu ya iliotajwa. Vipo vituo vinauza chini ya bei elekezi.
Hapo nakubali na pongezi zao. Lakini ni vichache mno.

Nchi nyingine hata wanakuuliza sababu zako za kuuza bei ya juu sana ni nini?
 
Nimezungumzia kiujumla ila kampuni husika ilitakiwa kupeleka malalamiko maana hizi taasisi hazifanyi kazi mpaka zipewe taarifa.
 
Taasisi ni nyingi Sana lakini lile jicho la kuona matatizo hawana, wao wanajua na kukariri basics tu.
 
Mitandao yote yasimu na hao FCC maana jamaa wote wanauza vifurushi vinavyo xpire pia bei zinazofanana
 
Kuna viofisi na vitaasisi ukiwekwa uko unakula adi unakufa na akuna atakaekuuliza uko maana akuna anaejua
 
Kuna viofisi na vitaasisi ukiwekwa uko unakula adi unakufa na akuna atakaekuuliza uko maana akuna anaejua
Kila siku wanaenda kazini wanapiga story wee,na huenda hata wanatongozana wee halafu wanarudi nyumbani. Nimeona kuna pisi kweli kweli hiyo ofisi! Sijui nani anipe kazi pale angalau ya udereva!
 
Kwa kweli matatizo ya ushindani wa kibiashara, kumlinda mlaji na biashara haramu ya bidhaa bandia ni matatizo "serious" sana katika jamii yetu.
Tatizo la eneo lile zipo kazi kwa uchache wake wanafanya ila hawahabarishi umma kabisa! Kurasa zao za mitandao zimejaa picha za viongozi na hawasemi wameshughulikia malalamiko kiasi gani, yapi yamesahihishwa na yapi bado. Umma ungeweza kufahamu milestone wanazozifanya japo kwa uchache. Eneo la kumlinda mlaji wanapaswa kuongeza jitihada zaidi walaji wanaumizwa sana na wafanyabiashara! Mfano katika eneo la warranty, mfabyabiashara anaweza kukataa tu kutoa redress kwenye product yake ambaye amekuuzia ukakuta ni mbovu. Walaji wengi hawajui waende wapi wala wafanye nini!! Tanzania haijawahi kufanya product recall (kwa batch la bidhaa zenye hitilafu zinazoingia sokoni!!). Bidhaa zinaingia sokoni hazina taarifa [product information], hazijulikani zinatokea wapi nani anatwngeneza yaani zipo tu na Sheria ipo kabisa inayokataza. Mimi mama yangu ashatumia budhaa kumbe ina ingredient ambazo sna allergy nayo. Hii ilitakiwa tupate angalau nafuu kutoka FCC. Ila taasisi zimeamua kuwa bubu. Haya bana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…