Tume ya Warioba 'imewatapeli' watanzania?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.

Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.

Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Akili za wabongo ni za kuhama hama sana!!!

Sikutegemea mzee Warioba aliyepigwa na watoto kwa maagizo ya wakubwa wao ambao wamepewa ukuu wa wilaya kwa kumpiga leo anakwenda watetea!!!

Akili za waafrika wengi bado zina vimelea vya utumwa!!!
 
Warioba alikuwa na haki ya kupokea kile kipigo. Tena wangemuongezea kabisa.
Na wanafiki kama kila Humphrey Polepole na makanjanja wengine waliokuwa wanaleta midahalo kumbe ni unafiki?
 
Akili ya warioba kubwa,ni kweli ametukanwa,ni kweli aridharaurishwa lakini tujiulize what is at stake in this coming elections,it is bigger than everything else ndo mana mheshimiwa warioba kaweka mbali everything else.alivyo weigh option zake akaona country wll be in better hands in CCM than Ukawa
 
bavicha kwa bifu bana.....jamani huyo mzee warioba ni mwanaccm,sasa kutofautiana na wenzake kuhusu katiba ni kitu cha kawaida,haina maana kuwa kishakua BAVICHA jamani.
tumieni akili basi,la sivyo kila siku mtakuwa mnanuna na kuanzisha nyuzi zisizo na mantinki.

polepole nae hakusema sasa amekuwa bavicha,ilitokea tu mkafananisha maoni kuhusu katiba
 
Usicheze na kitu pesa bana! Eti wamemwongezea Warioba mafao ya mwezi ndiyo mana amehuilishwa kiakili
 
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.

Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.

Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kwa hiyo ulikuwa unatakaje au unashauri nini? ?? Funguka kamanda. Lakini kabla ya hapo embu tueleze mbona Chadema wametutapeli kwa kutuaminisha Lowasa ni fisadi la kutupwa, mwishowake wanamshawishi aje achukue fomu ya kugombea urais na kumtupa nje Dr Slaa. Ujinga mtupu. Kweli siasa ni si asa!
Mnategemea utapeli mlioufanya utafanya wananchi watuamini tena. Wanatuona kama wajinga tu, usione watu wanakusanyika wengi kwenye mikutano mkadhani watatupigia kura. Ni ndoto ya mchana. Turudi tukajipange tena. Na ikiwezekana baada tu ya uchaguzi tumfukuze Lowasa na kundi lake na Mbowe wake na Mbatia. Turudi kwenye zama za ukweli za Dr Slaa na Lipumba basi.
 
Akili ya warioba kubwa,ni kweli ametukanwa,ni kweli aridharaurishwa lakini tujiulize what is at stake in this coming elections,it is bigger than everything else ndo mana mheshimiwa warioba kaweka mbali everything else.alivyo weigh option zake akaona country wll be in better hands in CCM than Ukawa
Well said. Tume ilitumwa na serikali kukusanya maoni na kuleta mapendekezo.. si lazima kila lilopendekezwa lifanyiwe kazi. Hii ndio maana ya demokrasia ya kweli na Mh. Warioba ni mtu anayeheshimika kitaifa na kimataifa ( alishiriki tume ya Umoja wa Mataifa ya maeno ya bahari) anajua nini ni muhimu kwa taifa kuliko majumuisho ya kamati. kama sehemu ya demokrasia alitofautiana na watu au chama chake lakini si yeye au chama kumfukuza kama vyama vingine vinafukuza wanachama wakitofautiana mawazo!
 
Akili za wabongo ni za kuhama hama sana!!!

Sikutegemea mzee Warioba aliyepigwa na watoto kwa maagizo ya wakubwa wao ambao wamepewa ukuu wa wilaya kwa kumpiga leo anakwenda watetea!!!

Akili za waafrika wengi bado zina vimelea vya utumwa!!!

Ulitegemea mbowe kuuza Chama!
 
Nipenda Maneno yako
 
Akili ya warioba kubwa,ni kweli ametukanwa,ni kweli aridharaurishwa lakini tujiulize what is at stake in this coming elections,it is bigger than everything else ndo mana mheshimiwa warioba kaweka mbali everything else.alivyo weigh option zake akaona country wll be in better hands in CCM than Ukawa

Warioba na Polepole hawataki tena serikali tatu. Mambo ya mshiko eeh. Polepole sasa anatetea hata lugha za matusi ya wazee wa CCM.
 
Akili ya warioba kubwa,ni kweli ametukanwa,ni kweli aridharaurishwa lakini tujiulize what is at stake in this coming elections,it is bigger than everything else ndo mana mheshimiwa warioba kaweka mbali everything else.alivyo weigh option zake akaona country wll be in better hands in CCM than Ukawa

Wewe una akili nyingi sana. Vijana wengine igeni mazuri yote ya Mwinchande84
 
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.

Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.

Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Siamini kama Warioba na wenziwe wanataka ccm irudi madarakani halafu waanze kuitetea tena 'kitabu' chao kwa watu walewale !
'Haiwezekani mpera kuzaa maembe'
 
Mbona pro-Chadema ndiyo wanaumia sana na Mzee Warioba, kwa akili za Bavicha wanadhani Mzee Warioba ni UKAWA.
 
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.

Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.

Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Anatengeneza maisha ya watoto wake.Naona mmoja amepata anagombea jimbo la kawe.

Mzee wangu tunacheza na ngoma ya CHUKI kati ya marafiki wawili ambao hawakukutana barabarani.Chuki ilianz kwao wawili,ikaenda ngazi ya familia,ikapita ngazi ya chama (tumezikia watoto wadogo wakimdhihaki na kumtukana)

Sikatai Lowassa ana mabaya kama binadamu lakini anayo mazuri mengi zaidi usikute kuliko baya lake moja la Richmond.
 
Akili za wabongo ni za kuhama hama sana!!!

Sikutegemea mzee Warioba aliyepigwa na watoto kwa maagizo ya wakubwa wao ambao wamepewa ukuu wa wilaya kwa kumpiga leo anakwenda watetea!!!

Akili za waafrika wengi bado zina vimelea vya utumwa!!!

Tofautisheni Katiba na uchaguzi...nani aliwaambia kuwa wajumbe wa Tume ya katiba ndiyo kuwa upinzani... nilitegemea mngemshukuru sana JK na mzee warioba maana bila wao hili dudu linaloitwa UKAWA msingekuwa nalo leo!
 
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.

Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.

Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kweli Warioba amesahau kuwa katiba aliyopendekezwa ilikataliwa na CCM Akiwemo Kufuli
 
Niombe radhi. Sijawahi kumuunga mkono Lowassa ingawa sibezi ushawishi na nguvu yake.

Mzee Tupatupa

Huna sababu ya kujustify kitu ili mtu mwingine akuelewe.Kama nilivyosema Lowassa ana mabaya na mazuri.

Kuna marais waitajirikia Ikulu nadhani ni wachafu kuliko Lowassa hawana hata morLs za kumnyooshea kidole Lowassa.Kuna waliouza NBC,mashirika ya umma yaliyokuwa yanafanya faida kubwa kwa bei ya kutupa kwa kisingizio cha wawekeaji.

Nikitafakari jinsi madini tulivyotupa kwa wakoloni eti wawekezaji unawapa asilimia 97,halafu unawaambia hawa mazuzu wape asilimia 3 na hPa naweka seal hakuna mtu kuiona mikata ni siri y mwekezaji.

Nikafikiria tusi la juzi eti Mzee wangu mimi Mpumbavu na lofa nikatafakari lile la miaka ile ati watanzania tunawivu wa kike,nikarudi mtaa wa Muhimbili wadi ya akina mama.

Mzee wangu nikafikiria na wale akina Warioba waliosimamia kidete ile Katiba yetu ghafla nikawaona wako meza moja wakipata John Walker na nyama choma na wale waliosigina Katiba yetu,nikafikiria sana nikaja na jibu hili::

Ni kweli Watanzania ni WAPUMBAVU NA MALOFA,tungekuwa wajinga tungejifunza toka kwa Mwinyi na Mkapa.Tungejifunza kutowaamini viongozi wa Katiba yetu Warioba,na Polepole.
Nikapata moyo na kusema hivi Mpumbavu na lofa:
1.Ni yule aliyeuza Mashirika yetu yote na Banki ya Taifa NBC kwa bei ya maandazi.
2.Ni yule aliyesaini mikataba na wakoloni aka wawekezaji kuchima madini yetu na kutuachia asilimia 3tu nyingine ni mali zao.
3.Tutakuwa Wapumbavu zaidi kama tukimchagua yule aliyeuza nyumba za serikali na kugawa nyingine kwa hawara,aliyenunua kivuko cha mwaka 1978 kwa biloni nane na kuacha kipya cha bilioni sita.Huyu aliyetuletea hasara ya kulipa wakandarasi hewa kwa bilioni 258.Anayetudanganya eti atatuletea milioni50 kila kijiji sijui atatoa wapi hakika lazima tuitwe wapumbavu na malofa maana ahadi zitolewzo leo zililetwa na BoyII mana miaka kumi iliyopita.

Hakika nitakuwa si Mpumbavu na lofa bali zuzu,mmana pesa ziliibiwa mikononi mwa huyi bora Lowassa wawili kuliko Makomea moja.
 
Kweli Warioba amesahau kuwa katiba aliyopendekezwa ilikataliwa na CCM Akiwemo Kufuli

dah. Mimi nilimshangaa sana mzee wangu warioba, alivyosimama na kumwaga sifa lukuki kwa, dada yangu, samia suluu hassan, kwamba ni mtu safi kabisa,

mimi nikasema hivi huyu mzee yupo kwenye ufahamu wake kweli?
Maana samia, ndiye alikua mwenye kiti msaidizi wa bunge la katiba!

Naalishiriki kuminya maoni ya wananchi?
 
Mkapa yeye ndio Lofa kabisa maana amesahau hata kwao kahamia Lushoto na amewasahau ndugu zake waliomsomesha kule mtwara bora hata membe kwa sisi wanamtwara kuliko huyo mzee
 
Back
Top Bottom