Tume ya Warioba yatishia kujiuzulu; Profesa Baregu, Kabudi, Butiku wawasha moto

Tume ya Warioba yatishia kujiuzulu; Profesa Baregu, Kabudi, Butiku wawasha moto

Kauli ya Chikawe kuwa JK asiposaini Muswada ataingia kwenye Mgogoro na Bunge haina Mashiko na ya kinafiki kama sio upotoshaji.
Alitakiwa aseme kuwa JK asiposaini Muswada ataingia kwenye Mgogoro na Wabunge Wanafiki na Wa Binafsi kutoka CCM na Mrema wa TLP
 
Watanzania wenye mapenzi mema na taifa letu wanapaswa kumuombea rais kikwete ili awe na hekima na busara hasa katika suala la katiba mpya! Kuna wahafidhina hatari sana ndani ya ccm hawana nia nzuri na kikwete kuelekea kupata katiba mpya, wao kazi yao ni kuhakikisha wanavuruga mchakato huu, hao wamejaa toka bungeni, kwenye baraza la mawaziri na hata ndani ya ccm kwenyewe! Katika hili watanzania tuwapongeze wapinzani kwa kuonyesha uzalendo zaidi kuliko vyama zaidi kuhusu katiba mpya!
 
Pole sana Rais Kikwete, tatizo kubwa ni mawaziri na mwanasheria mkuu wa serikali, wengi wao hapo uwezo wao wa kufikiri ni mdogo na wenye uwezo mzurio wa kufikiri hawana nia njema na serikali na wengine chuki binafsi na Raisi. Nakuomba raisi wangui Kikwete kuwa makini na mawaziri wako tena usiwaamini, naomba chukua muda wako binafsi na chunguza kwa makini nchi inaendaje, fuatilia mitandao ya kijamii utajua ukweli upo wapi.
 
Butiku anaelezwa kwenda mbali zaidi akisema amekubali uteuzi wa kuwa kamishna wa Tume hiyo si kwa sababu ya shida ya kupata pesa kwani amekwishazoea kuishi maisha ya bila kuwa na pesa, isipokuwa amekubali kuwamo kwenye Tume hiyo ili kujenga, kutetea na kulinda mustakabali bora wa nchi na vizazi vijavyo.


“Ndugu Mwenyekiti, sisi wengine tumeingia humo katika hii Tume si kwa sababu ya kupata pesa kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Butiku anataka kutuambia nini hapa?. Anatoa ujumbe gani kwa Watanzania?.

Sentesi yake kwa undani ina accuse some of the Commissioners of the Constitutional Review Commission kwa kuingia kwenye tume wakiwakilisha kwanza matumbo yao. Hao wengine walioingia kwa sababu ya kupata pesa ni kina nani?.

Kauli kama hizi zinaleta utata kwenye jamii inayoiangalia tume kama niya watu weledi ambao wako pale kwa sababu ya shinikizo la uzalendo na siyo shinikizo la ubinafsi.

Was it a slip of the tongue?.
 
Back
Top Bottom