Tume ya Warioba yatishia kujiuzulu

Tume ya Warioba yatishia kujiuzulu

Walichofanya wabunge wa CCM ni kujimaliza, bahati nzuri kura zilipigwa na wakaonekana bayana wakiukubali muswada. Ole wao wenye ndoto za kurudi tena bungeni iwe ni Bunge la Tanganyika au Jamhuri ya Muungano wa TZ.
 
...tukishindwa kuheshimiana kwenye haki za msingi tutachapana tu,na huu ndo ukweli. Hakuna kuzusha wapinzani wanavuruga amani wakati chanzo ni wao. Tuchapane tu ili heshima iwepo kama kenya...
 
Tume ya Warioba ni mwiba mchungu kwa msimamo wa ccm na serikali kwa ujumla. Kama itakuwepo kama refa, si magoli ya kuotea wala yale ya kufunga kwa mkono yatakayokubaliwa! Hii ni taabu kwa kuwa hiyo ndo mifumo ya ushindi wa ccm na serikali inapenda iwe hivyo.
 
ukitaka historia ikukumbuke kwa mazuri , hakikisha heshima yako na utu hauvunjwi.
 
...tukishindwa kuheshimiana kwenye haki za msingi tutachapana tu,na huu ndo ukweli. Hakuna kuzusha wapinzani wanavuruga amani wakati chanzo ni wao. Tuchapane tu ili heshima iwepo kama kenya...

Sina nywele kichwani kwa kufikiria tembo
 
mtoto wa kibajaji alisema demokrasia si ya wabunge wachache 49, sasa hawa wengine wanasema hata wachache au consesus ni bora.
 
Kwani moshi ulipoanza mbona walitonywa lakini wakajifanya hawaelewi sasa baada ya kushiba wanaanza.Wajiuzulu sasa maana uchaguzi wa makamati ya katiba watu walilalamikia sana lakini waliona yako sawa,sasa kwa nini waanze kupiga makelele?Wajiuzulu ndiyo tutaona kama ni kweli au wanatingisha kibiriti.
 
Muswada wa Sheria Rasimu ya Katiba: Hakuna anayebisha nadharia kuwa Demokrasia ni Wengi Wape. Watu wametoa maoni yao katika rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya. Hakuna kikundi chochote chenye sifa ya kubadili au kuacha waliyosema wananchi katika Rasimu ya Katiba. Nielewavyo, haja ya kujadili na kutoa maoni juu ya rasimu hii ni kutaka; (1) Tume kufafanua rasimu pasipoeleweka. (2) Kuboresha namna ya kutekelezaji wa yaliyomo katika rasimu na (3) Kuongeza chochote muhimu kilichoachwa katika rasimu na Katiba Mpya ( e.g. mipaka katika maziwa, n.k. kama wengine walivyodokeza) na kamwe siyo kutoa chochote kilichomo katika rasimu hiyo (kutoa chochote itahitaji baraka ya wananchi wenyewe vinginevyo ni uhaini kwa wananchi).
 
Chanzo cha mgogoro wa katiba ni wabunge wa ccm kutetea chama badala ya wananchi wao!
 
Hiyo Tume imeshaandika mustabali wa nchi hawataki kuburuzwa na watawala na pia hawataki aibu ya kupindisha haki iwe juu ya vipaji vya uso wao wako tayari kuondoka wasema fedha si amana ya wananchi wa Tanzania Bravo Mwenyekti wa tume na wajumbe wako simamieni haki ili tupate katiba mpya yenye malengo ya kusukuma gurudumu la maendeleo bila vikwazo
 
Nahisi aibu iliyopo, wasomi wenye elimu ya sheria na uelewa pevu katika maswala ya sheria na katiba, watakapo dumbukizwa kwenye lawama ya kuwatengenezea waTanzania katiba mbovu kwa ujumla..Binasfi naamini aibu hiyo,haitatokea, kwani ili cream ipatikane lazma patashika iwepo na nguo nyingi zichanike lakini mwisho wasiku katiba ya watu ikabidhiwe kwa nchi..
 
Back
Top Bottom