Tume yaondoa fomu za uteuzi wa Wagombea Urais kwenye Ubao wa matangazo

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
WhatsApp Image 2025-08-28 at 18.28.29_50dedee5.jpg
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima akiongoza watumishi wa Tume kuondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita Saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria.

Fomu hizo za Wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilibandikwa ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Fomu hizo zilibandikwa na Tume Saa 10:00 jioni ya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi na kuondolewa leo Agosti 28, 2025 Saa 10: 00 jioni.
WhatsApp Image 2025-08-28 at 18.28.29_78729d2a.jpg

WhatsApp Image 2025-08-28 at 18.28.29_63634361.jpg

WhatsApp Image 2025-08-28 at 18.28.29_e47ebaf7.jpg
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima akiongoza watumishi wa Tume kuondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita Saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria.

Fomu hizo za Wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilibandikwa ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Fomu hizo zilibandikwa na Tume Saa 10:00 jioni ya Agosti 27, 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi na kuondolewa leo Agosti 28, 2025 Saa 10: 00 jioni.
maana yaek ni nini?
 
Maigizo mengi, kwani kuondoa fomu ndio mpaka Muite waandishi?
 
Back
Top Bottom