DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
maigizo kila konaTUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema itawapatia waathirika wa vurugu hizo huduma ya kisaikolojia kutokana na madhila za vurugu hizo kwa kuwakutanisha na wataalamu wa saikolojia.
Baadhi ya waathiriwa waliofika na kutoa ushahidi wao ni waliojeruhiwa kwa risasi katika miili yao huku wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.
Mjumbe wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue ambaye anaongoza mikutano ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, alisema hayo wakati tume hiyo ikipokea ushahidi kutoka kwa makundi mbalimbali ya waathirika wa vurugu hizo katika Ukumbi wa Karimjee.
Makundi ya waathirika waliotoa ushahidi wao ni kundi ambalo ndugu zao walipoteza maisha, kundi lililopoteza ndugu zao na hawajui walipo, kundi la watu waliopata ulemavu na kundi la watu waliopoteza mali zao.
Balozi Sefue alisema baadhi ya wananchi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na vurugu hizo wanahitaji kupata ushauri wa kisaikolojia ili waikubali hali hiyo na maisha yaendelee na kwamba tume inatoa msaada wa kisaikolojia kwa kuwakutanisha na wataalamu hao.
Baadhi ya waathiriwa waliopata majeraha na ulemavu wa kudumu waliiambia tume kuwa kutokana na ulemavu huo walioupata wakiwa katika shughuli zao halali, walifikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.
“Hatuna uwezo wa kuwapatia miguu bandia lakini tunaweza kuwatafutia wataalamu wa saikolojia na kuwaunganisha na ninyi ili muweze kupata huduma hiyo na maisha yaendelee,” alisema Balozi Sefue.
Aidha, aliwasihi wananchi wanaofika kutoa ushahidi wa kitu gani kilitokea siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wasiwe na wasiwasi na kwamba maswali wanayoulizwa yanalenga kupata ukweli wa taarifa zinazotolewa.
Kadhalika, wananchi ambao biashara zao ziliathirika kutokana na vurugu za uchaguzi wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ili wahudumie familia zao kwa sababu mali zao ziliporwa na watu walioshiriki vurugu hizo.
“Biashara zangu zilizoharibiwa katika eneo la Buguruni, thamani yake inafika Shilingi milioni 42, naiomba serikali iangalie namna ya kunisaidia kwani sasa hivi nina miaka 53 nguvu za kutafuta na kuijenga biashara hii sina tena,” alisema mwananchi aliyepoteza maduka yake mawili Buguruni.
Mwananchi mwingine ambaye ni kiongozi katika ngazi ya Shina Mtaa wa Tabata, ameishauri serikali kuchukua hatua mapema baada ya kujitokeza viashiria vya uvunjifu wa amani ili kuokoa maisha na mali za wananchi.
Alisema kwa kuwa maandamano ni tiba ya mioyo ya watu, serikali iangalie namna ya kukaa na vijana katika zama hizi za kidijiti ili kujua mambo wanayowaza ama kuyatekeleza katika kujenga mustakabali wao au wanaotaka watekelezewe ili kuwa vijana wema kwa maslahi ya taifa.
“Serikali imetenga asilimia nne ya mikopo ya halmashauri kwa ajili ya vijana lakini ukifuatilia kwa undani hutakuta kijana hata mmoja aliyepata mikopo hiyo. Waziri wa Vijana atafute jukwaa la kukutana na vijana ili kujua hali halisi ya vijana na achukue hatua ili vijana waweze kuwafikia vijana,” aliongeza mwananchi huyo.
Chanzo: Habari leo
Pia soma ~ Matukio ya Uchaguzi Oktoba 29, yalivyoacha kovu la kisaikolojia: Nani wa kutoa msaada?
Tume imekuwa sirikali, hiyo nguvu, za kufanya hivyo wanazitoa wapi, mbona hawa zungumzi maiti zilizo zikwa , au ambao hawajapewa maiti za wapendwa wao. Mwisho Balozi na Jaji Mkuu Mstaafu walikuwepo kwenye Ile tume ya haki jinai ambayo haija tekelezwa Hadi sasa. Hawaoni kuwa Wana tumika vibaya nao ni watu wa Haki. Au wamebadilika sasa.TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema itawapatia waathirika wa vurugu hizo huduma ya kisaikolojia kutokana na madhila za vurugu hizo kwa kuwakutanisha na wataalamu wa saikolojia.
Baadhi ya waathiriwa waliofika na kutoa ushahidi wao ni waliojeruhiwa kwa risasi katika miili yao huku wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.
Mjumbe wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue ambaye anaongoza mikutano ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, alisema hayo wakati tume hiyo ikipokea ushahidi kutoka kwa makundi mbalimbali ya waathirika wa vurugu hizo katika Ukumbi wa Karimjee.
Makundi ya waathirika waliotoa ushahidi wao ni kundi ambalo ndugu zao walipoteza maisha, kundi lililopoteza ndugu zao na hawajui walipo, kundi la watu waliopata ulemavu na kundi la watu waliopoteza mali zao.
Balozi Sefue alisema baadhi ya wananchi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na vurugu hizo wanahitaji kupata ushauri wa kisaikolojia ili waikubali hali hiyo na maisha yaendelee na kwamba tume inatoa msaada wa kisaikolojia kwa kuwakutanisha na wataalamu hao.
Baadhi ya waathiriwa waliopata majeraha na ulemavu wa kudumu waliiambia tume kuwa kutokana na ulemavu huo walioupata wakiwa katika shughuli zao halali, walifikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.
“Hatuna uwezo wa kuwapatia miguu bandia lakini tunaweza kuwatafutia wataalamu wa saikolojia na kuwaunganisha na ninyi ili muweze kupata huduma hiyo na maisha yaendelee,” alisema Balozi Sefue.
Aidha, aliwasihi wananchi wanaofika kutoa ushahidi wa kitu gani kilitokea siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wasiwe na wasiwasi na kwamba maswali wanayoulizwa yanalenga kupata ukweli wa taarifa zinazotolewa.
Kadhalika, wananchi ambao biashara zao ziliathirika kutokana na vurugu za uchaguzi wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ili wahudumie familia zao kwa sababu mali zao ziliporwa na watu walioshiriki vurugu hizo.
“Biashara zangu zilizoharibiwa katika eneo la Buguruni, thamani yake inafika Shilingi milioni 42, naiomba serikali iangalie namna ya kunisaidia kwani sasa hivi nina miaka 53 nguvu za kutafuta na kuijenga biashara hii sina tena,” alisema mwananchi aliyepoteza maduka yake mawili Buguruni.
Mwananchi mwingine ambaye ni kiongozi katika ngazi ya Shina Mtaa wa Tabata, ameishauri serikali kuchukua hatua mapema baada ya kujitokeza viashiria vya uvunjifu wa amani ili kuokoa maisha na mali za wananchi.
Alisema kwa kuwa maandamano ni tiba ya mioyo ya watu, serikali iangalie namna ya kukaa na vijana katika zama hizi za kidijiti ili kujua mambo wanayowaza ama kuyatekeleza katika kujenga mustakabali wao au wanaotaka watekelezewe ili kuwa vijana wema kwa maslahi ya taifa.
“Serikali imetenga asilimia nne ya mikopo ya halmashauri kwa ajili ya vijana lakini ukifuatilia kwa undani hutakuta kijana hata mmoja aliyepata mikopo hiyo. Waziri wa Vijana atafute jukwaa la kukutana na vijana ili kujua hali halisi ya vijana na achukue hatua ili vijana waweze kuwafikia vijana,” aliongeza mwananchi huyo.
Chanzo: Habari leo
Pia soma ~ Matukio ya Uchaguzi Oktoba 29, yalivyoacha kovu la kisaikolojia: Nani wa kutoa msaada?
Kwenye vita siyo rahisi kujua maiti ziko wapi. Waliopata wana bahati ila waliokosa ndiyo tunaita Missing In Action.Kauli hiyo imetolewa n.a. Mjumbe wa Tume hiyo Ombeni Sefue
Bado haijafahamika namna matibabu hayo yanavyoweza kufanya kazi huku ikiwa bado baadhi ya marehemu hawajulikani waliko na kukiwa na tuhuma za makaburi ya halaiki kunduchi kwa kondo, Wala haifahamiki wale waliokatika miguu kwa risasi n.a. mabomu wataponaje kisaikolojia.
Bali bado haijahamika kama jambo Hilo ni miongoni mwa Hadidu za Rejea ilizopewa Tume hiyo Au La
Shetani hana rafikiKwenye vita siyo rahisi kujua maiti ziko wapi. Waliopata wana bahati ila waliokosa ndiyo tunaita Missing In Action.
Vita ya magenge ya wahalifu wa miundombinu ya Serikali dhidi ya TANPOL/ JWTZ haikuwa ya kitoto. Kama una ndugu yako humuoni nenda kachukue nguo zake na kuzika tu.
Haikuwa na namna zaidi ya risasi na Tanzania ni salama zaidi baada ya wale wahalifu kuteketezwa
Huyu shetani mnamuonea sana kwa kumsingizia vitu ambavyo hahusiki. Wale wahuni wameingia club ya The Voice pale Kinyerezi wakanywa pombe na kisha wakachoma bar!! Je huyo ni shetani aliwatuma?Shetani hana rafiki
Mzee Butiku ameanza project hiyo ya matibabu siyo. Ogopa teknolojia ya sasa, CCTV camera footage, satellite pictures and the likes.Kauli hiyo imetolewa n.a. Mjumbe wa Tume hiyo Ombeni Sefue