Tumeacha kujadili 'Budget' tumepewa Chalamila tumjadili

Hii bajeti ndiyo itakayomnyonga kwelikweli mnyonge na kupandisha gharama za maisha kwa hali ya juu kama mambo yasipokuwa managed vizuri tutegemee mfumuko wa bei
 
Mwanasiasa mmoja aliwahi sema 'Watanzania wana akili kama za kuku'
kuku huwa anatabia ya kusahau haraka sana. anaposogelea ama kula nafaka ya bosi wake, huwa anafukuzwa kwa kutumia ka sauti fulani hivi ambako huwa hakana madhara kwake. Haitachukua muda atarudi tena palepale alipofukuzwa. this time atafukuzwa kwa kurushiwa ama jiwe au kipande cha ukuni. lakini hata choka, muda mfui tena anarejea ili andelee kula nafaka ya boss wake. boss safari hii anaamua kumuumiza kabisa huyo kuku. Na mara nyingi huwa ni kutenguliwa baadhi ya viungo kama miguu, shingo, au mabawa. ataruka kwa sauti yenye kuashria maumivu makali kisha atakimbia. baada ya muda mfupi tu tena, atarudi akiwa amejeruhiwa huku akijivuta kuja eneo lilelile asilotakiwa kuwapo.

'Watanzania tunaumizwa mara nyingi mno na serikali yetu kupitia viongozi wetu, lakini hatujawahi kukumbuka na kufanya maamuzi mengine magumu ili kuepukana na maumivu hayo. Hata watesi wetu wanajua hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kulalamika kwenye mitandao' Tutaendelea kuumizwa kama kuku kila sikua kama hatutafanya maamuzi magumu sasa au hata hapo mbeleni.
 
Ngoja tuteme nyongo kwanza tutarudi baadae kuijadili
 
Elimu duni ya wananchi wengi ndiyo inawapa kiburi watawala ambao wengi wao pia ufisadi umewatawala

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Sio Hii wizara inaitaji
Burudani za Mama zimezidi utamu, anazidi kuwatengua Watesi wa Wananchi, Bajeti hata tukiijadili imeshapita.

Burudani! Burrudani! bado tu ya Professa Mussa Assad aishike Wizara ya Fedha halafu Lameck Madelu akafuge Fisi Iramba.
Sio siri hii wizara inaitaji mtu mtendaji alifikia mafanikio makubwa kama Asad,Kimei,siyo huyu alie ajiriwa kwenye fani yake ya uchumi mwaka sijui tena level ya chini ,mara yuko ofisa wa siasa chamani .elimu yote alionayo ya uchumi mpaka PhD niya darasani,hiyo experience ya economy ameipatia wapi na lini !!??
 
Na ashafahamu watanzania ni wepesi sana. Wanataka burudani. Wakija shtuka miaka imekatika hamna jipya.... [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ni staili ya uongozi wa JK hii!

Ilikuwa akiboronga yeye anapanda ndege huyoo ughaibuni au linatokea tukio ku cover lile la kuboronga mwishowe miaka yake 5 ikaisha
 
Nyie endeleeni kumjadili Chalamila ndio ana umuhimu kwenu
 
Unajua kuna baadhi ya wanaccm wanafikiri Nchi hii ni yao peke yao kuna nafasi ambazo Mama Samia anatakiwa aweke watu wenye uwezo bila ya kujali kama ni Makada wa Chama au la.
 

Wacha tudemke na chalamila
Tukimaliza mjadala wa bajeti umeisha
 
Bajeti inatajdiliwa na bunge... Sisi kazi yetu ni kupiga spana tu
 
Nmekwambia kwenye ule uzi mwaingine kwamba siyo kwamba ni kwa sababu bunge ni kibogoyo.

Ila shida watz ni wengi ni wajinga! Yani ishu ya kuathiri maisha yako kwa miaka 2 ijayo unaacha inapita hivi hivi ila likija suala la Chalamila na Diamond ndio watu mmekomaa hadi mishipa inawatoka.
 
Tukikomaa kama tunavyikomalia ishu ya Diamond na Chalamila wanaweza kubadili mawazo.

Mbona ishu ya gharama za vifurushi ilibadilishwa!
 
Leo hii ametenguliwa naona ni jambo jema. Lakini si suala la kitaifa kama la Budget. Hili ni la muhimu sana kujadiliana namna ambavyo wanaona ni bora kuwakata wananchi kodi kwenye Simcard na Kwenye Mafuta. Na tungeangalia athari zake kiuchumi.
Watanzania tuna matatizo sana
Kuna mtu alikuzuia usijadili budget?
Wewe mwenyewe umeongoza kumjadili chalamila kwa kumfungulia thread kabisa
 
Hivi kuna mtu kakuzuia kupost mjadala unaohusu bajeti hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…