Tumeambiwa hatuna matatizo ,tunaweza kupata mtoto, lakini mpaka sasa hakuna matumaini

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,293
Habarini wakuu.

Nimeona hili nilete humu manake majukwaa mengine watu wako bize na siasa najua humu lazima ntapata msaada wa mawazo.

Mimi ni me nimeoa nina mwaka mmoja na nusu sasa lakini katika kipindi hicho chote mke wangu hajabeba ujauzito.

Tumeenda hosp na kufanyiwa vipimo vyote wanasema wote hatuna matatizo tuendelee ku relax mimba itakuja tu.

Sikukata tamaa ikanilazima nitafte wana maombi kuna mama mmoja nikamualika atuombee hapa kwangu ndipo mapepo yalipolipuka kwa wife na kusema kuwa yametumwa na aunt yake yamfunge asizae. Huyo mama akapiga maombi kama masaa matano ivi ndo mapepo yakatoka na mama akatuambia tu relax mimba itaingia tu.

Sasa mzunguko wa wife ni siku 28 na jana ni siku yake ya 19 akaanza kulalamika tumbo na kiuno vinauma ndopo nilipoanza kumuombea maana nami pia nina imani. Nilipoomba akapandisha na mapepo yakaanza kusema kuwa yametumwa na shangazi kuja kuiharibu mimba ambayo imeshaingia.

Ikanilazimu kumuita jirani yangu nae ameokoka tukakemea balaa mpaka mapepo yakasalim amri kuwa yameshindwa yakakimbia.

Sasa leo ni siku ya 20 wife kaamka vizuri ila kila anapoona dalili za maumivu ananiambia namuombea yanaacha.

Wadau je kuna mtu hali hii ilishawahi kumtokea? Na je nini tiba ya kudumu kama kuna wadau wana vikundi vya maombi humu tutaftane tuunge nguvu huyu pepo asiharibu maana hakika nina ham sana na mtoto.

Sio stori ya kutunga ntaleta mrejesho kwa kila kinachoendelea manake nilishagaleta tatizo lang la kukosa mtoto hapa.

Wenye matatizo ya kupata watoto jamani komaeni kwenye maombi hasa kama umepima na kuambiwa huna tatizo shetani yupo jamani
 
Poleni sana,simama katika maombi na pia utoe sadaka kwa ajili ya ulinzi wenu,na hata ukimaliza kuomba hakikisha unafunga milango (kwa maombi) ili adui asipate kurudi tena,kwani hayo kurudi mara kwa mara inaashiria kuna mahali huenda mnajisahau na shetani anapata nafasi ya kuwasumbua,
 
Kama imani ipo 100%?!. Wewe tulia tu
 

umenena vyema mkuu hakika hapa ni kukazana tu na maombi nina amini shetani ameshashindwa
 

Cha msingi Ni mkeo kuokoka Tu!

Kama imani ipo 100%?!. Wewe tulia tu

mimi na mke wangu tumeokoka na tunaamini katika jina la Yesu ila imani zinazidiana wapo waliokirimiwa karama na vipawa zaidi
Hakuna cha kuokoka wala kuwa na imani hapo inatakiwa Huyo Shetani wa kutumwa Pepo Mchafu atolewe kwa Madawa na Mafusho Makali

ndipo Mke wako ataweza kusalimika na hiyo mimba itaendelea kukuwa pasipo na hivyo huyo Shetani wa kutumwa ataharibu hiyo mimba. Ukifanya maombi anakuja anakuambia maneno ya uongo nitatoka
 
Sijawahi kuona jambo gumu lakumshinda Mungu hata siku moja, achana na amani za kishetani hutafanikiwa zaidi yakukubadilishia huyo mtoto, upewe mtoto jini akusumbue hadi ujute kuzaa, mwombe Mungu pekee ndio atakae kusaidia
 
Relax tu babu, tafuta maji ya bange, vichwa tisa vya panzi, na meno mawili ya juu ya paka. Changanya vyote na weka juice kidogo ya madanzi. Mpe anywe. Kwisha kazi.
 

Mkuu umesema vema sana Step by step zingatia hili, simamieni pia neno hili Isaya 66:9.
 
Last edited by a moderator:
Kuwa na iman nakumbuka na mm nilikaa mwaka1 hakuna kitu kwa maombi ya watakatifu mambo yakawa safi.
 
Sijawahi kuona jambo gumu lakumshinda Mungu hata siku moja, achana na amani za kishetani hutafanikiwa zaidi yakukubadilishia huyo mtoto, upewe mtoto jini akusumbue hadi ujute kuzaa, mwombe Mungu pekee ndio atakae kusaidia

asante mkuu. Nimealika wachungaji wafanye maombi heavy na wengine wengi tu wanaendelea kuniombea online. Plz libebe hili pia unikumbuke katika dua zako
 
Relax tu babu, tafuta maji ya bange, vichwa tisa vya panzi, na meno mawili ya juu ya paka. Changanya vyote na weka juice kidogo ya madanzi. Mpe anywe. Kwisha kazi.

asante kwa ushauri ila sitaweza kuutekeleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…