Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Abdallah, Hasara Roho, D Timing, mtoto wa Kusini, mtoto wa Kiwalani, MTOTO WA MASKANI??
Mara ya kwanza nilimsikia kwenye ngoma yake iliyoitwa "Uwe Wangu" akimshirikisha Dully Sykes kwenye chorus na kuanzia hapo nikashawishika kumfuatilia.
Ngoma hii ilitengenezwa na Marco Chali akiwa Kama Kawa Production. Miaka kadhaa baadaye Chali akahamia MJ Records lakini "Akahama" na Dullayo na hapo wakaachia mkwaju ulioitwa "Bila yule" huku akishirikishwa "Bila Imani" na "Akili Maishani Utafeli", ukiunganisha herufi kubwa hizo utapata "Binamu", naam, Cousin Mwana FA.
Goma likafika mjini na kumtambulisha D kwa ambao hawakumfahamu au kwa ambao walikuwa wakimpotezea.
Wapenda muziki hawakukaa sawa, hapohapo MJ kwa Chali akaja Kesse Boy kutoka Mbeya na kumpa vesi Dullayo kwenye ngoma kali iliyoitwa "Kigoli", kufuru za kutosha zikafanywa na Q Jay pia humo ndani. Ngoma ililia sana kwenye radio airwaves. Hapo pia ikasikika "Saizi Yako" na "Nipumzishe".
"Mtaani Soggy Doggy, hommie, P the Mc
Mtaani Marco Chali, Za Chali, Beef Chali na haters nao chaliii
My people Dullayo and Lulle
We the army, coming motherf***** ya way" ni mamneno ya Wakazi kwenye ngoma yake iitwayo "Tanganyika" ikithibitisha kuwa Chali na D walitoka sehemu moja.
Chali akampotezea D, nakumbuka alilalamika sana redioni lakini ukweli ukasimama kuwa wasingefanya kazi tena. D akapotea.
Muda ukapita na D akarudi kwenye rotations akiwa na Producer Kisaka ambapo waliangusha mawe kama: Naumia Roho, Twende na mimi, Mida ya Kazi, Hawalali na Nimeamua.
Akaenda kwa Lamar na kugusa Kabongo Movie lakini pia akapita Sampamba Music na kufanya Jitambue, bonge moja la wimbo linalotia faraja moyo uliopondeka.
Akapita pia Togwe Records kwa Geoph Master na kuibuka na "Watu Wabaya". Kisha akaenda "Halisi Records" kwa Nature na kufanya Sina Papara. Lakini pia D alienda kwa KGT pale G Records na kufanya Kolabo na Zadao, goma liliitwa "Chocolate". D alipita pia kwa Mbezi na kufanya "Mchuzi Doa" akiwa na "Soprano" na "Black Ryno".
D anaonekana alikuwa anaamini katika kunyooka na producer mmoja. Akageukia kwa Zest na kuibuka na “Mara Mia” ft Ney Lee, Caro ft Beka Flavour na “Yule Yule” ft Raymond (Rayvanny) na kazi hii ilihusisha pia ubunifu wa Rashdon na ngoma bora zaidi iliyomwombolezea Ngwea iliyoitwa R.I.P Ngwea.
Watu wengi walimwandikia na kumwimbia Ngwea lakini hakuna aliyefika kwenye ubunifu na hisia alizozionesha D kwenye ngoma hii.
D alitengeneza combo nyingine kali na Producer Villy Nice ambapo waliangusha ngoma kali kama: Makavu Live ya X Dizo ft Dullayo, na Ommy G, Valentine, Superstar ft D Knob, 24/7 - x Dizo ft Dullayo, Baghdad na Nikki Mbishi, Maneno ft Easy Man na Ommy G, na Mokomoko ft Prof Jay.
D alisikika kwenye ngoma zifuatazo;
1. Oya - Soprano
2. Kila munu avena kwao- Kigwema
3. Nipe muda ft Q Jay
4. Makavu Live ft Joslin
5. Muziki na maisha - Lonka
6. Kwenye kona - X Dizo
7. Mchumba - Ommy G
8. Njoo unifariji - Chupa Sajo
9. Usiogope - Ney Lee
10. Tungi na misosi - Bwana Misosi
11. Nikuulize - PNC
Dullayo hakutofautiana na Ngwea kwenye kutaja details za nyimbo zake hususani kuhusu producers.
Dullayo na chama lake lililoitwa Makavu Live likiwa ni ushirika wa karibu wa Easy Man, Ommy G, X Dizo na Dullayo uliangusha makolabo kadhaa na kupotea kama haukuwahi kuwepo.
Miaka ya hapa kati nimeona videos kama mbili zikimchoresha Dullayo, niliumia sana.
Nimezungukia maandiko mengi yanayohusu game ya zamani lakini sikumbuki kama nimewahi kusoma andiko lililomhusu, ndipo nilipoamua kuuliza tumeamua kumpotezea Dullayo?
Nazikosa sana njia za Dullayo!
Luah, mwandishi wa aina yake.