Tumeanza kuishi kama wanyama, wakati wa ajali badala ya kusaidia watu waliopata ajali wanawaibia!

Jagwanana

Senior Member
Joined
Jul 3, 2024
Posts
130
Reaction score
224
Nilipata ajali ya gari Morocco bodaboda walikimbia kuja waliivamia wakaniibia kila kitu, pamoja jeki, tairi la gari, hela na kila kitu.

Juzi tu kuna mtu amepata ajali akagongwa na alikuwa na mshahara akiupeleka nyumbani kwa mkewe. Watu walimkuta na boxer tu hela wamebeba. Kila mahali kwenye ajali watu wanakimbilia kuumiza mwenye shida. Imekuwaje tumefikia hapa kama watanzania!
 
Pole sana mkuu
 
Umaskini,na ujinga hapo wamepungukiwa na maradhi tu,kuwa hamna kitu tena.
 
Usipozichukua mapema ambyulesi na polisi watamhifadhia pabaya.
 
Masikini ni kama mnyama
 
Wewe unasema hilo, unakuta baada ya ajali gari likipelekwa kituo cha polisi ukaliacha siku moja basi ukirudi unakuta kuna baadhi ya mali kwenye gari hazipo kama redio power window nk so hiyo ipo mpaka vituoni vya polisi unajiuliza aliechomoa ni nani, so uaminifu haupo kila mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…