bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Wakubwa shikamooni rika langu habarini za mchana.
Labda nianze kwa kisa hiki ili nipate kueleweka kisa chenyewe ni hiki hapa. Nlipata kusimuliwa na mtu wangu wa karibu sana juu ya raia wa nchi flani aliyekuja kwenye kikao Moshi ila mwisho wa siku komputa mpakato yake (laptop) ikaishiwa kukamatwa na wana usalama wa Tanzania ikiwa na michoro muhimu ya maeneo nyeti ya nchi yetu.
Niwape Kongole vyombo vyetu vya ulinzi kwa kufanya kazi iliyotukuta, ukiona mimi na wewe tunalala usingizi na kudamka salama, tunaenda kwenye shughuli zetu za uzalishaji na kurudi salama tukianza na Ulinzi wa Mwenyezi Mungu pia wapo wanausalama wetu wanayafanya kazi iliyotukuka nyuma yake.
Pamoja na wanausalama wetu kupiga kazi nzito ila bado kama taifa kuna kazi nzito ya kuendelea kuhakikisha taifa letu linakua salama leo, kesho na hata milele.
Siku za karibuni tumeshuhudia jirani na rafiki yetu DRC akinasa kwenye mtego wa waasi wa M23 na moja ya miji yake muhimu Goma kuangukia mikono mwa waasi na huku bado wakitamba watafika mpaka KINSHANSHA inaweza kuwa kweli au ni propaganda za kivita tu.
Swali la kujiuliza kama taifa tumepata funzo gani kupitia hilo., je tumechelewa kuchukua hatua au tumewahi
Kama taifa hatujachelewa wala hatujawahi kuna mengi ya kuendelea kufanya huku tukitambua ulinzi na usalama ni jukumu la kila raia mwenye mapenzi mema. Siku za karibuni tumeshuhudia mmoja wa watu muhimu akisema kuna watu toka mataifa mengine wamejipenyenza kwenye vyombo muhimu vya maamuzi ndani ya nchi yetu mimi na wewe hatujui kama yaliishia pale ua kuna hatua zaidi zilichukuliwa.
Adui yoyote ile ili akushambulie lazima akufahamu kwanza either kwa kutuma wapelelezi au kutumia faida ya mwingiliano wa raia, kwa hili la mwingiliano wa RAIA nahisi kama nchi tumejisahau sana imani tuliyonayo inatupa kiburi ipo siku tutajikuta tupo uchi mbele za maadui wetu.
Kutambua hilo nchi nyingi za jirani zimeingiza watu wake nchini mwetu na wakifika cha kwanza ni KUJIINGIZA KWENYE SIASA HASA KWA KUTUMIA CHAMA TAWALA WAKIFAHAMU FIKA WATAKUA SALAMA SALIMINI MPAKA MISSION ZAO ZITAKAPOKAMILIKA na kwa upendo wetu tunawapokea kwa mikono mizuri na kuwapa nafasi tena nyeti tu nafasi ambazo kule kwao huwezi sikia Mhaya, Mmakonde, Mhehe wa Tanzania kapewa.
Kiuhalisia maisha ya vijana wengi wa Tanzania hayana utofauti na vijana wa DRC kwanini nasema haya tumeshuhudia pale DRC wanajeshi wao wakisurrender hata bila kurusha risasi, Vijana wengi wa Tanzania leo hawana uzalendo na nchi yao, vijana wengi wanapenda starehe kamari, ulevi, ushabiki wa Simba na Yanga, Komedi za matusi tu na ushabiki wa Siasa usio na tija.
Hatuombei ila tujiandae ipo siku majirani zetu wataanzisha vita na sisi ikitokea jeshi letu limezidiwa na wanahitaji vijana wa kujiunga na jeshi wasipate vijana hata zaidi ya mia moja vijana wa sasa hawapendi mateso, vijana wamekosa uzalendo.
Ni ajabu kwa kijana mzalendo baada ya mkasa wa DRC wamevamia mitandaoni na kuanza kukejeli jeshi lao na kuanza kumsifu rais wa nchi flani na jeshi lake kwa jicho la mbali sio ajabu hawa vijana wanapokea mshahara toka nchi hiyo kwa kutumika kuuza propaganda.
Ni kijana wa Tanzania ambaye leo hajui propaganda za kivita ni kijana huyo huyo anayetaka jeshi lionyeshe zana zake ili yeye binafsi afurahi bila kujua hizo sio medani za kivita. Sio ajabu siku ya vita kijana huyo huyo akikutana na Air defence au vifaru vya jeshi atapiga picha na kuanza kupost mitandaoni bila kufahamu anamsadia adui.
Kama taifa kwa umoja wetu bila kujali itikadi zetu za kidini, kichama, kimpira na kisiasa kuungana kwa ulinzi na usalama wa Taifa letu, tuache propaganda zisizo na tija.
Angalizo tusomemeshe vijana tupate vijana wabobevu kwenye ishu za Propaganda kimaitafa leo hii unawaangalia vijana wanaotumika kupiga propaganda unasema moyoni hakika hapa kuna kazi propaganda zimegeuka na kuwa uchawa kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja au kakikundi flani.
Herini ya Mwaka mpya 2025.