Tumechoka kusikia kelele za CHADEMA

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
CHADEMA hebu jitathminini. Kama mmeshindwa kulinda haki yenu, kaeni kimya, acha CCM wasonge mbele. Kila kona ni malalamiko ya kuenguliwa kwa Wagombea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Unakuta wana CHADEMA mtaa mzima wamekusanyika wanalia kama watoto wadogo eti wameenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa serikali za mitaa/Vijiji. Mbaya zaidi, WANAUME wazima wanalia eti Afisa mtendaji mmoja tu amewaengua CHADEMA karibu wote.

Nimesema mara kadhaa, kama mmeshindwa kaeni kimya, inawezekanaje watu wazima anawaliza mtu mmoja tu, na ninyi bila aibu mnabaki kulia lia eti mmeenguliwa. CHADEMA, huo ni utoto.
 
Mbaya zaidi, WANAUME wazima wanalia eti Afisa mtendaji mmoja tu amewaengua CHADEMA karibu wote.
Watanzania wajifunze kupambania haki zao. Vinginevyo .....!!
 
Reactions: Lax
Na haswa makelele ya yule mpuuzi wa machame alihamia Arusha
 
Wewe ni mmoja kati ya wapuuzi wengi, endelea kufurahia uhuni unaofanywa na viongozi wako,mengine achana nayo
 
Nikuulize swali: Walipoitisha maandamano ulikwenda ?
Uliwahimiza /wahamasisha wangapi kwenda kwenye maandamano?

Now propose wafanyeje, wape la kufanya. If it were you, a Chadema authority for that matter, what would you have done in this situation of Tanzania brutal police and government!?
 
Kwanza sema wewe ndio umechoka, pili kwa misconduct hizo unata wakae kimya? Unataka walete vurugu halaf mseme chama cha hovyo?
acha walalamike ikiwezekana waende mahakamani
 
Kama umetumwa, waambie waliokutuma kuwa hatutaingia kwenye huo mtego!
 
Fanya yako wacha serikali ifanye yake unless we ni mwanasiasa
 
Kwanza sema wewe ndio umechoka, pili kwa misconduct hizo unata wakae kimya? Unataka walete vurugu halaf mseme chama cha hovyo?
acha walalamike ikiwezekana waende mahakamani
Haki huwa inapiganiwa. Haki haiji kirahisi rahisi hivyo.
Sisi huku kwetu hakuna aliyekatwa hata mmoja. Tuliwaambia kabla, wakati na baada ya kuchukua fomu kuwa, atakayethubutu kutuhujumu katika zoezi hili, awe tayari kutafuta Nchi ya kuishi kwa sababu Nchi hii itakuwa imemshinda.
Tuliendelea kuwakumbusha kwa kauli hii.
Kuna mmoja alijaribu kujichanganya tukamchanganya kisawa sawa. Baada ya hapo wengine wote wakashika adabu.
Hakuna mtu hata mmoja aliyekatwa.
Wakati mwingine DAWA YA MOTO NI MOTO.
 
gentleman,
umeeleza ukweli mtupu tena kwa hisia kali mno. wanapiga moyowe hadi wanaikera jamii 👊
 
Change channel tu mzee babaaa
 
Mmmh muongo wewe unajikosha tu hapa kwa sababu hatujui uko wapi, hebu lete ushahidi wa orodha ya wagombea tuone kama kweli wote wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…