TUMECHOKA NA MATUKIO , TUNATAKA KATIBA MPYA !!

TUMECHOKA NA MATUKIO , TUNATAKA KATIBA MPYA !!

Col FEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
327
Reaction score
460
Ndugu wana Jamvi naomba sasa tuwe serious /makini na Nchi yetu kwa faida yetu na ya vizazi vijavyo.

Tunahitaji kujenga Nchi yenye Matumaini kwa kila Mwananchi bila kuhitaji huruma za viongozi wetu. Nina chukia pale tunapo ishi kwa kutegemea huruma za viongozi wanao tuongoza bila ya kuwa na system/utaratibu ambao utakuwa Huru na wa Haki kwa kila Mtanzania kupata Haki yake stahiki.

Angalia sasa hivi kuna matukio kibao huku Wananchi tukibakia kushangilia na kubishana wenyewe kwa wenyewe. Nchi imekuwa ikiendesha na mtu mmoja , hakuna Bunge , Mahakama wala Serikali wote ni Bendera fuata upepo. Leo Mkuu akiamka na kusema wote mguu sawa basi nchi nzima ni mguu sawa ukipinga tu unaonekana msaliti na si mzalendo, Kesho mguu pande basi wote tunageuka. Watanzania tumekuwa kama "MISUKULE" Tunaendeshwa kama Mkuu anavyo taka. Hii ni hatari sana. Je huyu Mkuu ikiumwa ghafla Kesho mambo yatakuwaje ??

Je safari ya kuhamia Dodoma itaendelea ??

Je kuhakiki vyeti na elimu hewa kutandelea ??

Je kupambana na Rushwa na Ubadhilifu kutaendelea ??

Je sinema Makinikia itaishia wapi ??

Je watoto wanao pata mimba utotoni kwa kubakwa maisha yao Elimu watapata wapi ??

Je uhuru wa vyama vingi vya siasa upo wapi ??

Je Uhuru wa vyombo vya habari upo wapi ??

Je Kashfa ya Escrow itaishia wapi ???

Na mambo mengi ya matukio kibao tena ya kuanzishwa na mtu mmoja bila utaratibu maalum eti kwa faida ya watu zaidi ya 50mil.

Ndipo hapo natafakari na kuona Watanzania tumefanywa kuwa MISUKULE wala hatujitambui tumebakia kupiga mayoe tu... !!

Ushauri wangu kwa Watanzania wote Huu ni wakati wa Kudai KATIBA MPYA kwa faida ya sisi wenyewe na Vizazi vyetu vijavyo tushirikiane kwa pamoja, tuelimishane kwa ujumla wetu Mjini na Vijijini. Tuachane na hizi sinema za Matukio ambazo zimepangwa na Baadhi ya kundi la watu ili tu kujijenga Kisiasa na ili wapate kututawala kwa faida ya familia zao wakati Watanzania wengi tuko taabani kimaisha.

Tupate KATIBA Mpya yenye kujali Wakulima na Wafanyakazi wa Taifa letu la Tanzania. KATIBA yenye kutoa Haki kwa Watanzania wote , KATIBA yenye kuwangoza Viongozi na Kuwasimamia Viongozi wote ili wawajibike kwa Wananchi
Kisawa sawa bila kupindisha pindisha. KATIBA yenye kuwapa Wananchi Uhuru wa kweli siyo Uhuru bandia. KATIBA yenye kuwajibisha vyombo vya Usalama na Taasisi za Usalama zote Ziwajibike kwa Wananchi siyo kwa Chama Tawala.

NDUGU WATANZANIA TUUNGANE PAMOJA KUDAI KATIBA MPYA SASA.
 
mkuu tupige kazi katiba nahisi haitokutajirisha wewe bali ni juhudi binafsi na hata kama ukipewa raisi unaemtaka wewe bila wewe kujituma na kufanya kazi kwa juhudi zako huwezi kufanikiwa...siasa tuwaachie wanaoweza kutudanganya kua maisha bora yanapatika kukiwa na katiba mpya.
 
mkuu tupige kazi katiba nahisi haitokutajirisha wewe bali ni juhudi binafsi na hata kama ukipewa raisi unaemtaka wewe bila wewe kujituma na kufanya kazi kwa juhudi zako huwezi kufanikiwa...siasa tuwaachie wanaoweza kutudanganya kua maisha bora yanapatika kukiwa na katiba mpya.
Unaweza kuwa na ukweli, lakini mawazo yako yamejaa ubinafsi , lazima tuangalie mambo kwa ujumla wake kwa faida ya Taifa zima KATIBA nimuhimu sana kwa kila Mwananchi bila kujalisha Chama cha siasa , au itikadi fulani. Maendeleo yako Binafsi yatakuwa na Usalama kama Nchi itakuwa na misingi imara ya kiongozi la sivyo juhudi zako zinaweza ishia njia panda.
 
Back
Top Bottom