A
Anonymous
Guest
Sisi tuliokuwa wafanyakazi wa muda mrefu katika Hospitali ya JKCI-Dar Group (zamani ikijulikana kama Dar Group) tumejikuta katika hali ya sintofahamu kufuatia uamuzi wa mwajiri wetu kusitisha mikataba yetu ya kazi na kututupa kiinua mgongo licha ya kufanya kazi hapo kwa zaidi ya miaka 30.
Kundi la tulioondolewa kazini wengi wetu hatuna elimu ya juu, tunakubali hilo kwa kuwa umri wetu umeenda lakini basi wangetufikiria kuhusu kiinua mgongo.
Tulipewa barua tarehe 2 Aprili 2026, zikitutaarifu kuwa tutaondolewa kazini ifikapo tarehe 30 Aprili 2026.
Kiini cha Mgogoro
Baada ya kuondolewa wametulipa Mshahara wa mwezi wa nne (2026), malipo ya saa za ziada (extra duty) kwa wale waliofanya hivyo kwa mwezi husika, malipo ya likizo ambayo haijachukuliwa.
Tumeambiwa hakuna kiinua mgongo wala gharama za kusafirisha mizigo, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya awali na taratibu za kazi tulizozizoea."
Sisi hatulaumu wao kutuondoa kazini lakini kweli miaka yote hiyo hakuna kiinua mgongo? Baadhi yetu tumeanza kufanya kazi wakati taasisi ikiwa chini ya raia wa India, baadaye akaja mmiliki mwingine (Dkt. Mlingi) na sasa ipo chini ya Serikali, tukiwa katika nafasi ya Nursing Assistants.
Wapo wengine waliofanya kazi kwa miaka 40 kati yetu, wengine wachache ni vijana wadogo ambao walianza kazi hivi karibuni, mmoja wao ni mjamzito nao wameondolewa kaka sisi na hawajalipwa kiinua mgongo.
Tunaomba Serikali na uongozi wa JKCI -Dar Group utufikirie kuhusu stahiki hizo za kiinua mgongo, nafsi zetu zina vinyongo.
Walichojibu JKCI ~ Ufafanuzi kuhusu Wafanyakazi Wa JKCI – DAR GROUP ambao walisitishiwa Mkataba wa Kazi kutolipwa Mafao ya Kiinua Mgongo