Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Kadri muda unavyoenda ndivyo ninavyozidi kuelewa namna uchumi na tabia za wanunuzi zinavyobadilika.
Kwenye biashara kuna dhana mbalimbali zinazofundishwa, moja wapo ikiwa ni "Ignorance of Customer." Kwa lugha rahisi, dhana hii inahimiza mteja kufanya utafiti kabla ya kununua bidhaa au huduma ili asije akanunua kwa bei isiyo sahihi. Pia humfundisha mteja kwamba, inapowezekana, anaweza kufanya negotiation au kuomba discount.
Hiyo ni concept nzuri, lakini naamini watu wengi wameikariri vibaya.
Siku hizi watu wengi wanalazimisha kufanya bargaining kwa sababu tu wamekariri concept ya Ignorance of Customer. Kwao, kila bei wanayoambiwa lazima ipungue kwanza. Haijalishi bei hiyo ni ya haki, imepangwa kwa faida ndogo au tayari ni ya mwisho; wao wanaamini bila bargaining watakuwa wamefanya makosa kama wanunuzi.
Matokeo yake, bargaining power imeacha kuwa mbinu ya biashara na imegeuka kuwa tabia ya lazima.
Tatizo kubwa zaidi ni kwamba nguvu hii mara nyingi inaishia kuwaumiza wale walio chini kabisa kiuchumi.
Kuna watu wanaoishi kwa mfumo wa "hand to mouth." Wakifanya kazi leo ndipo familia yao inakula leo. Hawana mshahara wa mwezi wala akiba inayowapa nafasi ya kusubiri kesho.
Lakini cha kushangaza, hawa ndio wanaokumbana zaidi na bargaining isiyo na mipaka.
Ukienda kwenye site ya ujenzi, fundi akitaja labor charge yake, badala ya kujadiliana kwa haki, utaona wengine wanaanza kumwekea presha.
Kwa kuwa fundi anahitaji kazi ili familia yake ipate chakula siku hiyo, analazimika kushusha bei hata kama haitoshi kulingana na thamani ya kazi yake.
Viwandani nako hali ni hiyo hiyo. Watu wanafanya kazi ngumu kwa ujira mdogo, si kwa sababu kazi yao haina thamani, bali kwa sababu nafasi yao ya kujadiliana imekuwa ndogo sana.
Machinga nao hawajaachwa nyuma.
• Wamezunguka siku nzima kutafuta wateja.
• Wamebeba bidhaa kwa muda mrefu.
• Wametumia muda na nguvu kutafuta soko.
Lakini anapopata mteja, bado analazimishwa kushusha bei kiasi kwamba mwisho wa siku kinachobaki ni hela ya kula tu, huku biashara ikishindwa kukua.
Sisemi watu wasifanye bargaining.
Ninachosema ni kwamba bargaining inapaswa kutegemea mazingira, si kuwa sheria ya lazima kwenye kila ununuzi.
Kuna tofauti kubwa kati ya kubargain bei ya kampuni kubwa yenye faida za mamilioni na kubargain bei ya fundi, machinga au mtu anayepambana kutafuta riziki ya siku.
Wakati mwingine kulipa bei ya haki siyo kupoteza fedha; ni kuthamini kazi ya mwenzako na kumpa nafasi ya kuendelea kusimama kwa jasho lake.

"Kaka, hiyo bei ni kubwa. Kama umeshindwa nitatafuta fundi mwingine."