Why now!? Walikuwa wapi miaka yote 46 tangu tupate uhuru? Hawakuijua Tanzania miaka hiyo iliyopita sasa ndio wamesikia kwamba kuna kanchi kanaitwa Tanzania na ghafla tu wakajenga interest kubwa na nchi yetu!? Tuwaogope kabisa hawa urafiki wao ni wa undumila kuwili na historia juu ya urafiki wao ipo ya kutosha kabisa. Wanafukuzwa na wajapan kila kukicha lakini hawana mpango wa kuondoka. Wakiingia kwetu basi itakuwa ni balaa tupu maana tutakuwa hatuna uhuru wa kuamua lolote bila wao kulikubali au watajenga uadui na sisi.
Sasa hivi hakuna nchi hata moja ya kiafrika iliyowakubalia kujenga kituo chao cha kijeshi katika Afrika, sasa inaelekea wameitarget Tanzania ili wajenge kituo hicho. Pia kupatikana kwa uranium nchini kwetu na uwezekano wa kupatikana mafuta kumewafanya hawa jamaa wenye tamaa kubwa ya rasilimali hizo kufanya kila njia kuhakikisha rasilimali hizo ndani ya nchi yetu zinakuwa chini ya control yao. Kumbuka hawa Wairaq walikuwa ni rafiki zao wakubwa sana, mara tu walipokataa kuwasikiliza basi wakawa maadui.
Jeshi letu limefundishwa na Watanzania wenyewe na limeweza kupambana na nduli na kumtwanga vizuri sana pia linasaidia kulinda amani katika nchi mbali mbali duniani hivyo tuna jeshi zuri tu ambalo halihitaji mafunzo toka kwa hawa mandumila kuwili
Fungua macho uone history ya urafiki wa Marekani siku zote si urafiki wa kweli ndio maana negative attributes zao ni kubwa mno kuliko positive attributes hata katika nchi wanazoziita ni marafiki kama UK, France, Germany etc. Kama umesikia Hillary katika kampeni zake anasema kwamba kama akishinda basi Clinton atakuwu ambassador wa kujenga upya reputation ya marekani iliyobomoka all over the World. Open your eyes bro.
Ndugu yangu weeeee,
Hujui kuwa sasa kwa jirani zetu hapo mlango wa pili kunawaka moto? Huyu jamaa ni mjanja sana. Anakimbizia watoto wake kwetu. Na sisi tusipokuwa makini tutajuta majuto ya shetani jehanamu