#COVID19 Tumejipanga vizuri. Kupitia Corona tutaanza pata Misaada kama Uganda wafanyavyo

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Msema kweli mpenzi wa Mungu. Kwa sasa tunaanza kutengeneza hofu ya Corona ambayo haikuwepo. Muda mrefu sasa hatujapata tena taarifa kuwa watu wanakufa kwa Corona.

Labda sababu Dr. Magufuli alifariki na watu wamesahau tena habari za vifo vyote kuhusishwa na Corona. Leo hii yanatoka matangazo ya kuogofya watu n.k

Lengo ni nini? Tunahitaji pesa kupitia ugonjwa wa Corona. Hili lipo wazi kama ambavyo Uganda imeonekana Serikali ikipambana kuonesha Corona ipo hata kuzika Majeneza matupu. Huu ni mchezo wa kisiasa.

Tumeshaona hata zile mbwembwe za Mbowe kuvaa cloves kama dereva wa bodaboda hazipo siku hizi. Ameacha kuvaa barakoa. Anatembea ana kutana na wananchi kwa uhuru kabisa.

Ni nini kinachoendelea nchini? Corona inawezekana ikawepo kwa kiwango kidogo tu but naamini sasa itazidishwa kwa makusudi ili tuweze kidhi vigezo vya kupata pesa ambazo watu wachache watazipiga kama kawaida.

Huu ni uhuni ambao Watanzania tuukatae. Kama itaombwa misaada isiwe sababu ya Corona. Hizo pesa wanalipa maskini kwa kukatwa kodi za hovyo sana huku wanasiasa wakijitengenezea zaidi namna ya kula pesa za maskini.

Tutaanza kuona uhuni mwingi ukiandaliwa. Najua serikali yetu inataka pesa na inajua namna ya kula vizuri na wapinzani. Wananchi tutabaki wenyewe siku zijazo.
 
Acha tu wameshaamua hivyo,ili tuwe watumwa kwenye nchi yetu wenyewe kulazimishwa kuvaa barakoa hata huko Ulaya wamesha acha kuvaa,tumeona kwenye michuano ya Euro.
Tunajua watakuja na uongo was wimbi la tatu,kweli watatoa data za uongo ili kuwafurahisha watoa misaada ila wajue siku za usoni watajutia Sana uamuzi wao.Na mkono wa Mungu hautawaacha salama
 
Corona inatibiwa na nini? nyungu, barakoa, chanjo, malimao, maombi, au kutokuikumbuka/kuipotezea tu?
 
2813341_FB_IMG_1624005081350.jpg
 
Tumeshaona hata zile mbwembwe za Mbowe kuvaa cloves kama dereva wa bodaboda hazipo siku hizi. Ameacha kuvaa barakoa. Anatembea ana kutana na wananchi kwa uhuru kabisa.
Mbowe alisema ameshapata chanjo. Waliopata chanjo naona wanajiachia bila tahadhari hata huko ulaya
 
Mabeberu na benki zao wanataka kutukopesha ili watumiliki kwa madeni. Vikaragosi vyao nchini wanachotaka ni hela ziingie kusudi wapige. Walishajipanga awali kutoa huduma hewa kwenye lockdowns jpm akawakata maini.

Corona ni njama ya ubeberu wa kimataifa kutuibia na kuturudisha nyuma. Naona mama samia wajanja wanamchezesha game anasaliti msimamo wa kizalendo kukabiliana na wanyonyaji.
 
nchi za kiafrika kuendelea ni ngumu sababu tumekubali kuwa watumwa ndani ya nchi zetu wenyewe.
 
Nenda Hospitali ya Bugando ujionee kwa macho yako hali ilivyo. Hali siyo nzuri kabisa. Tuchukue tahadhari.
Hali sio nzuri mi nikajua hata nikienda Muhimbili au Amana nitakutana na hiyo hali isiyo nzuri.
 
Mabeberu na benki zao wanataka kutukopesha ili watumiliki kwa madeni. Vikaragosi vyao nchini wanachotaka ni hela ziingie kusudi wapige. Walishajipanga awali kutoa huduma hewa kwenye lockdowns jpm akawakata maini.
Corona ni njama ya ubeberu wa kimataifa kutuibia na kuturudisha nyuma. Naona mama samia wajanja wanamchezesha game anasaliti msimamo wa kizalendo kukabiliana na wanyonyaji.
zidisha maombi usije kukutana nayo aisee!! Kama uko karibu na Mpango, muulize
 
Msema kweli mpenzi wa Mungu. Kwa sasa tunaanza kutengeneza hofu ya Corona ambayo haikuwepo. Muda mrefu sasa hatujapata tena taarifa kuwa watu wanakufa kwa Corona.

Labda sababu Dr. Magufuli alifariki.na watu wamesahau tena habari za vifo vyote kuhusishwa na Corona. Leo hii yanatoka matangazo ya kuogofya watu n.k

Lengo ni nini? Tunahitaji pesa kupitia ugonjwa wa Corona. Hili lipo wazi kama ambavyo Uganda imeonekana Serikali ikipambana kuonesha Corona ipo hata kuzika Majeneza matupu. Huu ni mchezo wa kisiasa.

Tumeshaona hata zile mbwembwe za Mbowe kuvaa cloves kama dereva wa bodaboda hazipo siku hizi. Ameacha kuvaa barakoa. Anatembea ana kutana na wananchi kwa uhuru kabisa.

Ni nini kinachoendelea nchini? Corona inawezekana ikawepo kwa kiwango kidogo tu but naamini sasa itazidishwa kwa makusudi ili tuweze kidhi vigezo vya kupata pesa ambazo watu wachache watazipiga kama kawaida.

Huu ni uhuni ambao Watanzania tuukatae. Kama itaombwa misaada isiwe sababu ya Corona. Hizo pesa wanalipa maskini kwa kukatwa kodi za hovyo sana huku wanasiasa wakijitengenezea zaidi namna ya kula pesa za maskini.

Tutaanza kuona uhuni mwingi ukiandaliwa. Najua serikali yetu inataka pesa na inajua namna ya kula vizuri na wapinzani... Wananchi tutabaki wenyewe siku zijazo.
Kule Uganda wananchi wamelalamika kuwa serikali inadanganya kuwa watu wanakufa na corona ilihali wanazika majeneza matupu ili kuwadanganya wafadhili kwa ajili ya kupata fedha.
 
Nenda Hospitali ya Bugando ujionee kwa macho yako hali ilivyo. Hali siyo nzuri kabisa. Tuchukue tahadhari.

Hao kuelewa heri kenge kusikia. Huo ndiyo urithi wetu tokea kwa yule aliyetangulia.
 
Back
Top Bottom