Tumekaa zaidi saa moja tunasubiri kwenye kituo cha mwendokasi Msimbazi

Prince Luanda

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
2,255
Reaction score
2,825
Kwenye kituo cha mabus ya kutoka gerezani kwenda Mbezi Mwisho abiria tumejaa tu humu mabus yanatupita hadi watu wamepaniki na kuwatupia lawama walinzi wa kituo.
 
Mnawanea tu walinzi wa kituo, sio kazi yao hiyo.

Au kila mnyonge na mnyonge wake, hapo akija hata mkuu wa wilaya kuwasikiliza hiyo kero yenu kila mmoja ataufyata, mkitembea na biti la mama kaupiga mwingi..

Hapo zuieni gari moja tupu, au zuieni kabisa gari zinazoingia tupu na kuondoka tupu bila ya kubeba abiria.
 
Mwendokasi mimi binafsi naona ni ubabaishaji, pesa inayotumika kujenga hizi barabara mpya za Tegeta na nyinginezo zingekutumika kununua mabasi ya kutosha kufeed hiyo morogoro road na kilwa road.. then baadae ndo waendelee kujenga...
 
Mabasi yanapita yakiwa tupu sasa abiria wanahoji ina maana walinzi hawaoni huu umati kwa nini wasisimamishe mabasi abiria wapandw?
 
HUu mradi kama umejifia tu hakuna namna tena, madereva hawana maadili na utu kabisa.
 
Mwendokasi mimi binafsi naona ni ubabaishaji, pesa inayotumika kujenga hizi barabara mpya za Tegeta na nyinginezo zingekutumika kununua mabasi ya kutosha kufeed hiyo morogoro road na kilwa road.. then baadae ndo waendelee kujenga...
Wenzenu wanajenga ili wasikae kwenye foleni na ninyi, watembee kwenye barabara za mwendokasi kuwahi waendako
 
Tuma picha broo Ili Uzi upendeze Gali likija likiondoka tupu piga picha tupia humu
 
Mabasi yanapita yakiwa tupu sasa abiria wanahoji ina maana walinzi hawaoni huu umati kwa nini wasisimamishe mabasi abiria wapandw?
Daah mnawaonea bure kabisa walinzi, mnawapa changamoto kubwa sana aisee.

Wao kazi yao ni kuhakikisha ninyi mnapanda mabasi au usalama wenu muwapo hapo kituoni?? Route za mabasi anazijulia wapi? Yeye ndo anapanga basi hili liende huku na hili likapakie pale??

Mlinzi ndo mmepa hela zenu, ndie kawapa tickets??
Mnamuonea tu, si ajabu hata hajui hilo tatizo akaliripoti wapi...

Kaba hao wakatisha tiketi, zuieni gari tupu la sivyo mtaishia kutukana kama kawaida yetu wabongo.
 
Huu mradi wanaosimamia ndio wanaharibu. Ebu fikiria dereva anachoma mafuta kuanzia ferry hadi kimara gari tupu kwa kuwa kajisikia tu.
Yaani madereva wake wanajisikia kama miungu, kwamba abebe abiria asibebe mwisho wa mwezi atapokea tu mshahara. Yani wasimamizi nagari yana camera, wanashindwa kukagua na kuwajibisha madereva wanaochoma mafuta bure.

Hizi gari zingekuwa kama zile UDA kuwa kila dereva ana konda na nauli anakusanya mwenyewe na kupeleka hesabu nadhani akili ingewakaa.

Nanyi abiria msiwe wanyonge, kadaini hela zenu, yani msiwachekee muone kama hawataita gari hapo. Mi nishawadai nauli Mara 2 kivukoni, na wakanipandisha gari hazina abiria zaidi yangu, na madereva walivyo mazuzu, kunishusha kituoni wanafungua mlango wa mbele ili abiria wasipande.
So nikiwakuta abiria wamejaa kituoni naonaga wanajitakia. Jitoeni ufahamu hapo wafanyieni timbwili muone.

Uzuri pana camera, msivunje chochote, we ukifika dai nauli, yani komaa nauli yako tu wakurudishie. Mkienda 10 lazima akili iwakae.
 
We jamaa mtata kama username yako 😂
 
Kwenye kituo cha mabus ya kutoka gerezani kwenda Mbezi Mwisho abiria tumejaa tu humu mabus yanatupita hadi watu wamepaniki na kuwatupia lawama walinzi wa kituo.
Hivi yule muwekezaji wa kiarabu yuko wapi, si walisema wanampa hiyo huduma aifacilitate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…